Kamati
za Kudumu za Bunge zitaanza kukutana Jumatatu tarehe 11 hadi 31 Machi, 2019
Mjini Dodoma kutekeleza majukumu ya kibunge kabla ya Mkutano wa Kumi na Tano wa
Bunge uliopangwa kuanza tarehe 02 Aprili, 2019. Kwa mujibu wa Ratiba ya
Shughuli za Kamati, Waheshimiwa Wabunge wote wanapaswa kuwasili Mjini Dodoma
Jumapili tarehe 10 Machi, 2019 tayari kwa ajili ya kuanza kwa vikao vya
Kamati.
Shughuli
zitakazotekelezwa na Kamati hizo ni pamoja na:
1.
KUPOKEA
WASILISHO LA SERIKALI KUHUSU KIWANGO CHA UKOMO WA BAJETI.
Katika
kipindi hicho cha vikao vya Kamati za Bunge, siku ya tarehe 12 Machi 2019,
Wabunge watapokea Wasilisho la Mapendekezo ya Serikali kuhusu Mpango na Kiwango
cha Ukomo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa mujibu wa Kanuni ya 97 ya
Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016.
1.
KUFANYA
ZIARA ZA UKAGUZI WA MIRADI
Kamati
zitafanya ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo iliyotengewa fedha katika
Bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa mujibu wa Kanuni ya 98(1) ya Kanuni za Bunge
Toleo la Januari, 2016.
Kamati zitakagua miradi ya uwekezaji liyotekelezwa na
Serikali kupitia Mashirika ya Umma. Aidha, Kamati ya Hesabu za Serikali
(PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zitafanya ziara za
ukaguzi wa miradi mingine iliyotekelezwa na Serikali ili kulinganisha matokeo
ya utekelezaji na thamani halisi ya fedha za Umma zilizotumika katika miradi
hiyo.
1.
KUFANYA
UCHAMBUZI WA BAJETI
Katika
vikao hivyo pia Kamati zitafanya uchambuzi wa Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti
za Wizara inazozisimamia kwa Mwaka wa Fedha unaoishia 2018/2019 kwa ajili ya
kufanya ulinganisho kuhusu makadirio ya matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha
2019/2020 kwa mujibu wa Kanuni ya 98(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la
Januari, 2016.
1.
KUFANYA
UCHAMBUZI WA TAARIFA ZA UWEKEZAJI
Kamati
ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) itafanya uchambuzi wa Taarifa za Uwekezaji
uliofanywa na Serikali kupitia Mashirika ya Umma kwa mujibu wa Kifungu cha 12
cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016.
1.
UCHAMBUZI
WA SHERIA NDOGO
Kamati
ya Sheria Ndogo itafanya uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa wakati wa
Mkutano wa Kumi na Nne Bunge kwa mujibu wa Kifungu cha 11 cha Nyongeza ya Nane
ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari, 2016
Ratiba
zote za Shughuli za Kamati za Bunge ikiwa ni pamoja na maeneo ambayo Kamati
hizo zitafanya ziara zinapatikana katika Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz.
mara baada ya Kamati hizo kuanza kazi.
Imetolewa
na: Kitengo cha
Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa.
Ofisi ya Bunge
DODOMA
05
Machi, 2019
No comments:
Post a Comment