Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
anaondoka nchini leo kuelekea Kampala, Uganda kushiriki kwenye Mkutano wa mwaka
2019 wa ‘Africa Now Summit’unaotarajiwa kufanyika tarehe12 na 13
Machi.Mhe. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Mkutano huo
utafunguliwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambaye ndiye
mwenyeji wa mkutano huu. Mkutano utakuwa na mada mbalimbali ikiwemo ya Uongozi
unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi Afrika, mada hii
itatolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan.
Viongozi
wengine watakaotoa mada ni Rais wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa
Afrika (UA) Mhe. Abdel Fattah el Sisi; Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril
Ramaphosa; Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. William Ruto; na Waziri Mkuu wa
Ethiopia Mhe. Ahmed Abiy. Mada zote hizi zitajikita kwenye kuonesha chachu ya
Uongozi katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika.
Mkutano
utamalizika tarehe 13 Machi 2019 utaanza na hotuba kutoka kwa Rais wa Somalia
Mhe. Mohamed Abdullahi na baadae kufungwa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Uganda
Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.
Makamu wa
Rais ataambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.
No comments:
Post a Comment