Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na
serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo kushoto akimpa maelekezo Mkuu wa
Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa kulia kuhusiana na usimamiza wa fedha
zinazotolewa katika miradi mbali mbali ya maendeleo katikati ni Mbunge wa Jimbo
la Kibaha vijijini Homoud Jumaa mara baada ya kukagua ujenzi wa wodi tatu zilizojengwa
katika kituo cha afya mlandizi pamoja na kujionea ukarabati wa
chumba cha kuhifadhia maiti.
...................................
VICTOR MASANGU, KIBAHA
WAZIRI
wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani
Jafo amechukizwa kuona baadhi ya viongozi na watendaji kutotimiza majukumu yao
ipasavyo ikiwemo kufanya mambo kienyeji kwa kupokea miradi ya maendeleo pasipo
kufahamu mwenendo mzima wa mkataba ulivyo pamoja na kutojua gharama za
fedha ambazo zinatolewa kwa ajili ya utekelezaji.
Jafo
ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kituo cha afya cha
mlandizi kilichopo Wilayani Kibaha mkoani Pwani kwa lengo la kujieneo mwenendo
mzima wa ukarabati wa majengo pamoja na kujionea ujenzi wa majengo matatu
ambayo yamejengwa kwa kiasi cha shilingi milioni 400 fedha ambazo zimetolewa na
serikali kuu.
Pia
Jafo alibainisha kuwa hawezi kuwavumilia watumishi ambao ni wazembe na
wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo na kuwataka kuachana mara moja na
vitendo vya kujihusiha na ubadhilifu wa fedha ambazo zinatolewa na serikali kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo.
“Mimi kama kiongozi wetu sipendi
kuona kabisa mnafanya kazi kienyeji bila ya kuzingatia sheria na taratibu
amabzo zimewekwa na nchi, na katika hili siwezi kulifumbia macho maana maeneo
mengine
nimepita nimekuta miradi mingine bado inasua sua nah ii ni baadhi ya
watu kutotimiza majukumu yao ipasavyo ni ninachotaka miradi yote inapokuja
lazima wahusika kufahamu mikatab ailivyo pamoja na fedha ambayo inatolewa sio
kupokea tu,”alisema Jafo.
Aidha
aliseama kwamba serikali ya awamu ya tano kwa sasa imeshatoa fedha katika vituo
vya afya zaidi ya 90 hapa nchini kwa lengo la kuweza kuongeza
majengo mengine pamoja na kufanya ukarabati wa miundombinu ya wodi mbali mbali
ikiwemo nyumba za watumishi kwa lengo la kuweza kuboresha sekta ya afya kwa
wananchi.
Aidha
katika hatua nyingine Jafo ameupongeza uongozi wa halmashauri ya Kibaha
vijijini kwa kutekeleza agizo lake la kukukarabati chumba cha
kuhifadhia maiti katika kituo cha afya mlandizi ambapo hapo awali kilikuwa
hakifanya kazi kabisa kwani kiligeuzwa kuwa eneo la stoo na kuhifadhia
vyuma chakavu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kibaha vijijini
Butamo Nuru alisema kwamba wametekeleza agizo ambalo walipatiwa na
waziri wa Tamisemi la kukarabati miundombinu ya chumba cha kuhifadhia maiti
pamoja na kununua majokofu nane ambayo yamegharimi kiasi cha shilingi
milioni 36.
WAZIRI
Jafo katika ziara yake ya kikazi kwa halmashauri ya Kibaha vijijini
ameweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa majengo
matatu ya wodi ya upasuaji,wazazi,na wagonjwa wa nje (OPD) sambamba na
kutembelea miradi mingine miwili ya ujenzi wa hospotali pamoja na jengo
la ofisi za halmashauri hiyo.
Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman
Jafo kushoto akimpa maelekezo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wa
kulia kuhusiana na usimamiza wa fedha zinazotolewa katika miradi mbali mbali ya
maendeleo katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Homoud Jumaa mara
baada ya kukagua ujenzi wa wodi tatu zilizojengwa katika kituo cha afya
mlandizi pamoja na kujionea ukarabati wa chumba cha kuhifadhia maiti.(PICHA
ZOTE NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment