NA
HADIJA HASSAN-LINDI
JUMLA
ya Wasichana elfu 4000 kutoka Halmashauri ya manispaa ya Lindi na Nachingwea
Mkoani Lindi wanatarajiwa kufikiwa na Mradi wa lishe kwa watoto wa kike (GIRLS
POWERD NUTRITION) unaoendeshwa na World Association of girls guide and
girl scouts
Hayo
yameelezwa na Meneja wa Mradi huo David Mbimila leo Machi 31, 2019 wakati wa
ufunguzi wa mafunzo ya kuwajewajengea uwezo wa usimamizi wa Mradi huo kwa
Viongozi wa Girl Guide wa Manispaa ya Lindi
Mbumila
alisema Mradi huo wa Lishe kwa watoto wa kike Duniani unafanyika kwa
majaribio katika Nchi tano ikiwemo Tanzania, Bagladesh, Sirilanka,
Filipino na Madagaska
"kwa
Tanzania Mradi huu unatekelezwa katika Mikoa sita ikiwemo Mkoa wa
Dar-es-salaam, Tanga , Arusha, Lindi , Dodoma pamoja na Mkoa wa Mara
ambapo kwa Mkoa wa Lindi kwa kuanzia tutaanza na Halmashauri ya Manispaa ya
Lindi pamoja na Wilaya ya Nachingwea ambapo matarajio yetu ni kuwafikia
wasichana elfu nne mpaka ifikapo 2020" alifafanua Mbimila
Mbimila
aliyataja malengo makuu ya Mpango huo kuwa ni kutoa Elimu ya Lishe kwa watoto
wa kike ili waweze kula vizuri, kukua vizuri, kuongeza nguvu kazi ya kitaifa
Alitaja
malengo mengine ni kutaka kuishahuri Serikali kuweka Mada ya Lishe kwa Watoto
wa kike katika vikao na mikutano yao wanayoifanya mara kwa mara , pamoja na
kulipa kipaumbele swala la lishe kwa Mtoto wa kike katika Sera na Sheria
Mbali mbali ambazo wanazitengeneza
Nae
kamishina wa Girls Guide Mkoa wa Lindi Grecy Chipanda alisema kuwa kati ya
wasichana hao elfu 4000 watakaonufaika na Mradi huo wasichana 2700
watatoka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi huku 1500 watatoka Wilayani
Nachingwea
"unaweza
ukajiuliza ni kwanini Wasichana wengi wametoka Manispaa hii ni kwa sababu
Viongozi wengi wa Mkoa tuko hapa , kwa hivyo bira shaka kwa kushirikiana kwa
pamoja na viongozi wa Wilaya tunaweza kuunganisha nguvu zetu na kufanikisha
mpango huu kufanyika vizuri" alisema Chipanda
Nae
Mwenyekiti wa Girls Guide Mkoa wa Lindi Mwalimu mstaafu Zuhura Mohamedi alisema
kuwa Baada ya mradi huo wa Lishe kwa watoto wa kike wa majaribio
kumalizika mwaka 2020 matarajio yake ni kuona wasichana Wanashiriki kikamilifu
katika masomo yao pasipokukosa kuhudhuria Darasani
Alisema
matarajio yao mara baada ya kumaliza kwa warsha hiyo walimu pamoja na viongozi
wa girls guide walioshiriki mafunzo hayo wataenda kuwaelimisha wanafunzi pamoja
na jamii kwa ujumla umuhimu wa kula chakula chenye lishe bora ili kumaliza
changamoto zinazowakuta wasichana hasa wa umri kuanzia miaka 6 hadi 19
Awali
akifungua warsha hiyo ya siku nne katibu tawala , utawala na rasilimali
watu wa Mkoa wa Lindi DKT Bora Haule alisema kuwa kama Mkoa wamefarijika
kuona Mkoa wao ni miongoni mwa Mikoa sita inayotekeleza mradi huo, huku
akieleza kwamba Mradi huo utakuwa unaunga mkono jitihada zinazofanywa na mkoa
huo za kuongeza ufaulu kwa Watoto wakike sambamba na kutokomeza mimba za
utotoni kupitia kampeni ya "TUMSAIDIE AKUE, ASOME, MIMBA BAADAE"
Pamoja
na mambo mengine Dkt Bora pia aliwataka washiriki wa Mafunzo hayo kwenda
kuwajibika kikamilifu katika maeneo yao sambamba na kuwataka Wananchi wa
Manispaa ya Lindi na wa Wilaya ya Nachingwea kuupokea mradi huo pamoja na
kuwapa ushirikiano wa kutosha waratibu wakati wa kutekuleza Mradi huo
No comments:
Post a Comment