Na Mwandishi wetu
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza mamia ya watanzania katika
kongamano la kujadili namna ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto,
kongamano litakalofanyika tarehe 22-23 March, 2019 katika ukumbi wa Chuo Kikuu kishiriki
cha elimu (DUCE) Jijinii Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake, Mkurugenzi wa Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Bw. Koshuma
Mtengeti amesema katika kongamano hilo la Kitaifa jumla ya mada sita zitnatarajiwa
kujadiliwa.
Ametaja mada hizo kuwa ni kujadili hali
ya ukatili kwa watoto katika familia na mashuleni, ukatili wa kijinsia na
unyanyasaji, mimba za utotoni na ndoa za utotoni. Zingine ni Ukeketaji, malezi
katika ulimwengu wa kisasa, ukatili wa kingono katika taasisi za elimu ya juu,
ukatili dhidi ya watoto kwenye mitandao na namna ya kuwapatia msaada waanga wa
vitendo vya ukatili.
Akizungumzia maandalizi ya Kongamano
hilo, Mtengeti amesema kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa na kwamba
wanaamini Kongamano hilo litaleta chachu ya kutokomeza vitendo vya ukatili
dhidi ya wanawake na watoto.
Amesema Kongamano hilo linaloandaliwa kwa
ushirikiano na , Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF chini ya udhamini wa ubalozi
wa Uswisi pamoja na shirika la C SEMA na chuo kikuu kishiriki cha elimu (DUCE) litaibua
Mijadala mizuri kwa sababu na wataalamu wa tafiti pia wameshirikishwa katika
hili.
Ameongeza kuwa kupitia kongamano hilo
viongozi wa kitaifa, watafiti, Asasi za kiraia, Wanataaluma, Viongozi wa Dini,
wanaharakati wa haki za binadamu pamoja na wadau wa maendeleo watapata fursa ya
kujadili hali ya ukatili na namna ya kuimarisha mikakati ya kutokomeza ukatili
dhidi ya wanawake na watoto.
Ukukubwa wa tatizo la ukatili
dhidi ya wanawake na watoto
Akifafanua hali ya ukatiliiiiiii dhidi
ya wanawake na watoto, amesema kwa mujibu wa utafiti wa demografia na afya wa
mwaka 2015/2016, idadi ya wasiichana wanaopata watoto katika umri wa shule ya
msiingi (miaka 15-19) imeongezeka hadi kufikia 27% mwaka 2015 kutoka 23% mwaka
2010.
Pia utafiti huo unaonyesha kuwa
wanawake wenye umri kati ya Miaka 15-49 wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa Kimwili
tangu wakiwa na umri wa miaka 15. Kati yao 17% wamefanyiwa ukatili wa kingono, 50%
walio kwenye ndoa nao wamepitia ukatili wa kingono wakiwa na umri wa miaka 15.
No comments:
Post a Comment