Saturday, March 16, 2019

Mrithi wa Maalim Seif CUF aomba radhi...atema cheche, asema anaanza na hili


 

Mrithi wa nafasi ya Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamadi hatimaye amepatikana mapema hii leo, lakini Katibu huyo ameomba radhi kwa wale wote waliokwazika katika kipindi cha mpito walichopitia na kuwataka kuwa kitu kimoja ili kukijenga Chama Chenye Nguvu ya kushika dola.
Amesema wakati wa kurumbana umekwisha kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii ya kukifanya chama kiwe chenye kuaminika na hatimaye kushika dola, jambo ambalo ni dhamira ya Chama chochote cha Siasa.
"Nimepanga kuanza na kuleta umoja ndanii ya chama, nitallisimamia hilo, mimi na wenzangu tutafanya kazi bila kuchoka kukifanya chama hiki kinapata hadhi yake, ndiyo maana nawaomba radhi wale wote tuliowakwaza, ilikuwa ni njia Mungu ametupitisha lakini mwishowe tumefika. Kwa wanachama wa CUF, nataka niiwaambie kama walikuwa wanapenda mtu basi huyo mtu sasa hayupo lakini kama wanapenda Chama basi chama chao kipo imara na kitafanya kazi zaidi ya zamani" Aliongeza Khalifa Suleiman Khalifa
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemtangaza Khalifa Suleiman Khalifa kuwa katibu mkuu wa chama hicho.

Mbali na Khalifa, Profesa Lipumba pia amemtangaza mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya kuwa naibu katibu mkuu Bara na Fakhi Suleiman Khatibu kuwa naibu katibu mkuu Zanzibar.

Profesa Lipumba amemtangaza Khalifa ambaye ni mbunge wa zamani wa Gando kuchukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad leo Jumamosi Machi 16, 2019 makao makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam.

Katibu mkuu huyo mpya, amepatikana baada ya kuchaguliwa na Baraza Kuu la Uongozi lililokutana jana Ijumaa.

Hata hivyo, hatima ya viongozi hao wapya wa CUF akiwamo Profesa Lipumba aliyechaguliwa na mkutano mkuu Jumatano iliyopita Machi 14, 2019, itajulikana baada ya hukumu itakayotolewa Jumatatu ya Machi 18, 2019 na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.

Hukumu hiyo ni ya kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wanachana wa chama hicho upande wa Maalim Seif wakipinga uhalali wa Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti wa CUF.

No comments:

Post a Comment