Dar
Es Salaam
Spika
za masikioni maarufu kwa jina la “Headphones” zimetajwa kuwa chanzo
kinachopeleka tatizo la usikivu hafifu kwa watu.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri mwenye dhamana ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na wananchi katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Jijini Dar Es Salaam katika kuadhimisha
siku ya usikivu duniani.
Waziri Ummy amesema kuwa matumizi ya simu za kisasa yameongeza kasi ya watu kutumia spika za masikioni jambo ambalo linahatarisha kuwa na watu wengi wenye matatizo ya usikivu.
“Unakuta kijana kuanzia asubuhi mpaka jioni ameweka spika za masikioni anasikiliza muziki hawajui wanajiweka katika hatari ya kupata tatizo la usikivu” amesema Waziri Ummy na kuendelea kusema kuwa kundi la vijana liko hatariki kupata matatizo ya usikivu.
Waziri
Ummy ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kupunguza matumizi ya spika za
masikioni ili kuweza kujikinga na matatizo ya usikivu.
“Nitoe
rai kwa vijana wapunguze matumizi ya spika za masikioni kwa muda mrefu, tusipo
kuwa makini tunaweza kujikuta tuna taifa lenye watu wengi wenye matatizo ya
kutosikia vizuri” amesema Waziri Ummy.
Aidha,
Waziri Ummy amesema kuwa tatizo la usikivu hutokea pia kwa njia mbalimbali
ikiwemo kwa kuzaliwa na tatizo hilo au kulipata ukubwani kutokana na sababu
nyinginezo ambazo zinaambata kwa kukaa kwa muda mrefu kwenye sehemu zenye
kelele nyingi pamoja matatizo yanayoambata na afya ya sikio.
Waziri Ummy amesema kuwa ni jambo jema kuona sasa matibabu ya matatizo ya
usikivu hafifu yanapatikana hapa hapa nchini huku akiwataka wananchi kukata
bima za afya ili kuweza kupata matibabu kwa uhakika.
“Serikali
imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha tatizo hili linazuiliwa kabla ya kutokea
lakini pia kuhakikisha matibabu yanapatikana yakiwemo kutumia mashine ya
mawimbi ya sauti, upasuaji wa kuziba tundu la ngoma ya sikio pamoja na
kupandikizwa vifaa vya kusaidia kusikia” amesema Waziri Ummy.
Hata hivyo alisema takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2018 Hospitali ya Muhimbili imefanikwa kuwapatia wagonjwa 116 vifaa vya mawimbi ya sauti, wagonwja 43 walifanyiwa upasuaji wa kuziba tundu la ngoma ya sikio.
Waziri
Ummy amesema kuwa Serikali itaendelea kuboresha huduma za matibabu ya kibingwa
na kuhakikisha matibabu yanapatikana hapa hapa nchini.
Awali
akitoa taarifa yake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Bw. Makwaiya Makani amesema kuwa wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali katika
eneo la usikivu ikiwemo kutoa huduma ya upandikizaji vifaa vya usikivu kwa
Watoto wenye matatizo ya hayo.
“Tangu mwezi Juni mwaka 2017 tayari watoto 21 wamepandikizwa vifaa vya usikivu kitaalam kwa jina la 'cochlear implants” amesema Bw. Makani
“Tangu mwezi Juni mwaka 2017 tayari watoto 21 wamepandikizwa vifaa vya usikivu kitaalam kwa jina la 'cochlear implants” amesema Bw. Makani
Bw.
Makani amesema kuwa wameendesha kliniki ya siku mbili katika Hospitali ya
Mloganzila kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya matatizo ya usikuvu ambapo
watu 264 wamejitokeza kati yao watu 172 walihitaji uchunguzi zaidi wa usikivu,
watu 64 wamekutwa na matatizo ya usikivu na tayari wamepatiwa rufaa kwa ajili
ya matibabu zaidi na watu 31 wamekutwa na nta za masikioni,pia watu 26
wamekutwa na maambukizi kwenye masikio ambao wamepatiwa rufaa ya matibabu
zaidi.
Tatizo
la usikivu linazidi kuongezeka siku hadi siku. Inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia
5 ya watu duniani wana tatizo la usikivu. Tatizo hili litaongezeka maradufu
kila mwaka. Inatakiwa kila mmoja achukue hatua kujikinga na tatizo hili ikiwemo
kuepuka sehemu zenye kelele na pia kusikiliza mziki kwa sauti kubwa na kwa muda
mrefu na kwa kutumia spika za masikioni.
No comments:
Post a Comment