NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
WAHAMIAJI haramu 12 raia kutoka Ethiopia ,wamekamatwa
mkoani Pwani, eneo la Mwidu porini, Chalinze kwa kosa la kutokuwa na kibali
kinyume na sheria.
Aidha watu 14 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo
kwa makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo wizi wa pikipiki na kukutwa na
madawa ya kulevya aina ya bangi.
Akielezea juu ya matukio hayo, kamanda wa polisi mkoa wa
Pwani,ACP Wankyo Nyigesa, alisema usiku wa kuamkia march 8 ,askari polisi
walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu uwepo wa wahamiaji hao
waliojificha kichakani eneo la Mwidu barabara ya Dar es salaam -Morogoro.
Alieleza baada ya polisi kufika eneo hilo waliwakamata
wakiwa safarini kutoka Ethiopia kuelekea Afrika ya Kusini.
:”Baada ya mahojiano ilionekana watu hao walifichwa hapo na
mtu ama watu ambao bado hawajafahamika kwa lengo la kuwatafutia usafiri wa
kuelekea nchini Afrika Kusini kutafuta ajira. “
Hata hivyo Wankyo alibainisha, afya ya wahamiaji haramu hao
walikuwa wamedhoofika.
Wakati huo huo jeshi hilo linawashikilia watu nane kwa
kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo wizi wa pikipiki.
Pia watu sita wamekamatwa kwa kupatikana na dawa za kulevya
ikiwemo bangi kete 172.
Wankyo alielezea kwamba, baada ya mahojiano na upelelezi
kukamilika watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment