Vijana
wa Morogoro wametakiwa kuchangamkiaa fursa za kilimo zilizopo katika Mkoa huo
ili kujiwezesha kujiinua kiuchumi
Hayo
yamebainishwa na Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba wakati akizungumza katika
uzinduzi wa Jukwaa la Vijana wa Mkoa wa Morogoro uliohudhuriwa na Vijana wa
Mkoa huo pamoja viongozi mbalimbali
Naibu
waziri Mgumba amewataka Vijana hao kuchangamkia fursa hizo ikiwepo kupata mkopo
kutoka Bank ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na mikopo ya Matractor
kutoka Shirika la Maendelo la Taifa (NDC) Pale Kibaha ili kuweza kujiari katika
sekta hiyo.
Alisema
kuwa Mkoa wa Morogoro umepata bahati ya kuwa na viwanda vikubwa ambavyo
vinahusika katika sekta ya Kilimo ikiwemo Kiwanda cha Mtibwa Sugar,
kilombero sugar, Mkulazi one na two, Mansoor industry cha kutengeza Sigara,
ujenzi wa Kiwanda cha kukoboa Mpunga na Kiwanda cha kuchakata mazao ya
jamii ya Mikunde cha Mahashree
Naibu
waziri wa Kilimo Omary Mgumba amewataka Vijana kutosubiri ajira tu za kuajiwa
ofisini na badala yake waungane kwa pamoja kwa kuanzisha mashamba, kushiriki
katika ujasiliamali wa mazao ya kilimo, kutoa huduma kwenye sekta ya kilimo na
kuongeza thamani ya mazao ya kilimo ili kutengeza ajira kwao vijana na kuajiri
vijana wenzao na kuweza kujikomboa kiuchumi.
Akizungumza
na mamia ya Vijana wa Mkoa wa Morogoro katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Waislam
MUM mkoani Morogoro Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba amewahakikishia Vijana
kuwa serikali chini ya Mh Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuwakomboa
wakulima kupitia mazao ya Kimkakati program aliyoizindua mwaka Jana na Mhe
Raisi Dkt. John pombe Magufuli kubadilisha kilimo toka cha kujikimu na kuwa cha
kisasa na cha kibiashara.
Mgumba
ameongeza kuwa ni vyema Vijana hao wakashirikiana na wataaalam mbalimbali ili
kuhakisha wanalima Kilimo chenye tija, na kujiunga kwenye Vikundi na kwenda kuomba
ardhi serikali za vijiji na kuzipima kupata hati za umiliki ardhi zitakazo
tumika kwa ajili ya uzalishaji mali na kuwa dhamana kwenye taasisi za fedha
kupata mitaji ya kuwekeza kwenye kilimo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe amesema kuwa Mkoa
huo umebarikiwa kutokana asilimi kubwa ya mazao mbalimbali kustawi vizuri.
Dkt.
Kebwe alisema kuwa Mkoa huo pia una ardhi kubwa ambayo inafaa kwa kilimo
ikiwemo cha umwagiliaji kutokana na kuwepo na mito mingi ambayo itamuwezesha
mkulima kulima kwa kipindi chote.
Hata
hivyo ametumia fursa hiyo kuwapongeza Vijana wanaohitimu chuo kikuu cha Kilimo
SUA kwa jitihada zao za kujiingiza katika Kilimo na kutosubiri ajira za
serikali.
Jukwaa
la Vijana Mkoa wa Morogoro limezinduliwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI Suleiman Jafo ambapo amewataka Vijana hao kuhakisha wanatumia vyuo vya
Kilimo vilivyopo katika Mkoa huo kubalidisha hali ya Mkulima.
Jukwaa
hilo la Vijana Mkoa wa Morogoro limezinduliwa likiwa na kauli mbiu "Fursa
Zetu Mkoa Wetu"
No comments:
Post a Comment