Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo,akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) leo jijini Dodoma .
......................................
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo,amesema kuwa Serikali
imetoa fursa ya wiki mbili kwa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha tano
kufanya mabadiliko ya machanganuo ya tahasusi na kozi mbalimbali walizochagua
kwenye fomu ya F4 Selform.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani
Jafo,wakati akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake amesema kuwa wiki
hizo mbili zitaanza mwezi wa Aprili Mosi hadi 14 mwaka huu.
Aidha Jafo amesema kuwa fursa hiyo ni
ya kwanza kutolewa mwaka huu na ni mara ya kwanza ambayo itawawezesha wanafunzi
kurekebisha mchanganuo huo kulingana na ufaulu walioupata katika matokeo ya
kidato cha nne ya mwaka 2018 yaliyotolewa na Baraza la Mitihani Tanzania
(NECTA).
Waziri Jafo amesema kuwa kuanzishwa
kwa mfumo huu ni moja ya maboresho yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano
katika kuhakikisha sekta ya Elimu inakua kwa kasi na kumpa fursa kila
mwanafunzi aliyefaulu kujiunga na kidato cha tano au chuo.
Hata hivyo amesema kuwa
hali hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi ambao hawakujaza vizuri tahasusi zao
kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu.
”Ofisi yangu inatoa fursa hii kwa
wahitimu kubadili mchanganuo ili kutoa mwanya zaidi kwa wanafunzi kusoma fani
au tahasusi itakayomwandaa kuwa na utaalamu fulani kwenye maisha yake ya baadae
kwa nafasi yake ambayo anatamani yeye mwenyewe au kwa kushauriwa na wazazi au
walezi wake ”amesema Jafo
Hata hivyo amesema Ofisi yake tayari
imeshakamilisha zoezi la awali la kuingiza taarifa zilizo kwenye Selform za
wanafunzi kwenye kanzidata ya Tamisemi na mabadiliko hayo yatakayofanyika kwa
njia ya mtandao yakikamilika kanzidata hiyo itatumika kuwachagua na kuwapangia
kidato cha tano na kozi za vyuo.
”Kwa mwanafunzi yeyote atakayekuwa
hajabadilisha taarifa zake mpaka muda kuisha Ofisi yake itaamini kuwa wanafunzi
huyo ameridhika na machaguo yake ya tahasusi aliyoyafanya hapo awali alipokuwa
shuleni” amesisitiza Jafo
Mtandao wanaotakiwa kuutumia ni
kuomba ni www.selfom.tamisemi.go.tz
ambao amesema kuwa upo wazi tangu wakati huo.
No comments:
Post a Comment