Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimwa Zainabu Kawawa, akiwa ameshika mfano wa hundi ya milioni 338.3 kwaajili ya vijana na wanawake Halmashauri ya Chalinze.
Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimwa Zainabu Kawawa, akizungumza na wana vikundi vilivyopata mikopo hiyo.
.....................................
Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimwa Zainabu Kawawa, amekabidhi hundi yenye thamani
ya Fedha za kitanzania milioni 338.3 zilizotolewa na Halmashauri ya
Chalinze kwa vikundi 64 vya Vijana na wanawake kwa robo ya pili ya mwaka wa
Fedha wa 2018/2019.
Fedha hizo ni asilimia 10 ya Mapato ya ndani yanayo kusanywa
na halmashauri hiyo
Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika uwanja wa polisi
Chalinze ambapo Mkuu huyo wa Wilaya katika hotuba yake ya kukabidhi hundi aliupongeza
uongozi wa halmashauri ya Chalinze kwa kuheshimu na kutii maelekezo ya serikali
kwa kutenga asilimia 10 ya Mapato ya ndani na kuwakopesha wanawake, vijana na
walemavu.
Hata hivyo Kawawa alihimiza ukusanyaji wa Mapato ya halmashauri kwa kuwataka wananchi na wataalamu kuziba mianya yote inayoweza kusababisha upotevu wa Mapato na kusababisha miradi mbalimbali ya maendeleo kutotekelezeka hivyo kukwamisha utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi.
"Mikopo hii ya wanawake
na Vijana itatekelezeka kwa sababu ya juhudi ya ukusanyaji wa Mapato
inayoendelea, ndiyo maana miradi yetu katika maeneo mbalimbali inaendelea
kutekelezwa. "Kawawa alisema.
Akitoa ufafanuzi wa taarifa hiyo katika hafla ya ugawaji hundi kwa wanawake na Vijana, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze Bwana Shabani Millao alieleza kuwa robo ya pili ya mwaka wa Fedha 2018/2019 halmashauri hiyo imetoa kiasi cha shilingi milioni 338.3.
Alisema fedha hizo zimetolewa ili kutekeleza bajeti na maagizo ya
serikali ya kuwakwamua vijana na wanawake katika lindi la umasikini wa kipato
kwa kuwakopesha asilimia kumi ya makusanyo ya Mapato ya ndani ya halmashauri.
Aidha Millao alieleza kuwa mpaka sasa takribani miaka mitatu tangu ianzishwe halmashauri ya Chalinze imekwisha toa mikopo kwa wanawake na Vijana jumla ya Fedha za kitanzania milioni 967 kwa vikundi 257.
Aliongeza kuwa, hali hiyo inawawezesha Vijana
na wanawake kujiajiri wenyewe kutokana na shughuli za ujasiriamali
wanazozifanya kutokana na mikopo hiyo.
"Halmashauri ya Chalinze mpaka sasa
haina deni lolote kwa upande wa Asilimia 10 ya Mapato ya ndani yanayo takiwa
kupelekwa kwa wanawake na Vijana tunatekeleza kwa kadiri tunavyokusanya na
kuisimamia bajeti kwa mujibu wa sheria." Millao alisema.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya Jamii anayeratibu vikundi Bi Wahda Mwishehe aliwataka wanawake na Vijana kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali ili waweze kukopesheka kwa urahisi na kuwataka warejeshe mikopo kwa wakati ili mikopo hiyo waweze kukopeshwa na wengine.
“ Akinamama wenzangu tuweni waaminifu
kwa kurejesha mikopo mliyochukua kwa wakati kwani mambo yamekuwa rahisi kwa
sasa kwani serikali imeondoa riba kwa wanawake na Vijana wanapokopeshwa na
halmashauri, Mwishehe alifafanua.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Mhe Saidi Zikatimu alieleza kwa kina mafanikio ya halmashauri yake katika ukopeshaji fedha kwa vikundi vya wanawake na Vijana kwa kusema kuwa kwa halmashauri ya Chalinze kutoa mikopo siyo tatizo bali wanawake na Vijana kutounda vikundi kwa wakati ili kupatiwa mikopo hiyo.
Zikatimu alitoa rai kwa maafisa maendeleo wa halmashauri kuwafikia wanawake
na Vijana katika vijiji vyao na kuwapa Elimu ya namna ya kujiunga katika
vikundi na kuwaelewesha mchakato mzima wa namna ya kupata mikopo,
"Fedha
tunazo tunahitaji Vijana na wanawake wajitokeze kuomba mikopo na mikopo hii
haina riba kiasi cha Fedha atakachokopeshwa mlengwa ndicho atakachorudisha“.
Zikatimu alieleza.
Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimwa Zainabu Kawawa akiwakabidhi wawakilishi wa vikundi katika halmashauri ya
Chalinze hundi hundi ya milioni 338.3.
No comments:
Post a Comment