Mbunge
wa chaline Ridhiwani Kikwete akikagua mradi wa kisima kirefi alioujenga kwa
pesa yake katika shule ya sekondari mboga ili kuwaondolea changamoto ya maji
walimu na wanafuni wa shule hiyo.
...................................
Na
Shushu Joel,Chalinze.
MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani
Ridhiwani Kikwete amefanikiwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na
salama iliyokuwa ikiwakabili walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Mboga
iliyodumu takribani kwa kipindi cha miaka zaidi ya 10 tangu kuanzishwa kwa
shule hiyo.
Akizungumza
mara baada ya kukagua na kujiridhisha kwa ujenzi wa mradi huo wa maji ya kisima
kirefu kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa shule hiyo, mbunge huyo alisema kuwa
Jimbo la chalinze kwa ujumla linachangamoto kubwa ya maji lakini juhudi za
uchimbaji wa visima virefu kwa ajili ya taasisi kama shule na za afya
zinafanyika ili kutokomeza uhaba huo kwenye maeneo hayo.
“Maji
ni uhai kwani kila kiumbe hai kilichopo hapa duniani kinahitaji maji safi na salama ili
kiweze kuishi hivyo ni jukumu langu kama kiongozi kuhakikisha maji safi na
salama yanapatikana kwa asilimia kubwa katika jimbo la chalinze”Alisema
Kikwete.
Aliongeza
kuwa ni kipindi kirefu walimu na wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakikumbwa na
changamoto ya ukosekanaji wa maji lakini kwa kuanzia tumeanza na upatikanaji
huo wa kisima kirefu ili pampu zitakuwa zinasambaza maji kwenye pointi
zilizotengwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali shuleni hapo.
Pia
amemtaka mkuu wa shule hiyo kuhakikisha miundombinu ya maji hayo yanalindwa ili
kisima hicho kiweze kudumu kwa muda mrefu na si kukiharibu kwa makusudi ili
mbunge aweze kutoa hela ya kukarabati.
Aidha
Ridhiwani Alisema kuwa huduma hiyo ya upatikanaji wa maji si tu kwa ajili ya
walimu na wanafunzi wa shule ya mboga bali itakuwa ni mkombozi wa upatikanaji
wa huduma hiyo ya maji katika eneo hilo hivyo wananchi nao wanapaswa kupata
nafasi ya uchotaji wa maji kijijini humo
kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Kwa
upande wake mkuu wa shule hiyo ya Mboga sekondari Lunge Mwalaba amempongeza
mbunge Kikwete kwa juhudi zake anazozifanya katika jimbo la chalinze kwa ujumla
katika shughuli za ukamilishaji wa maendeleo kwa wananchi,kwani kilio cha
upatikanaji wa maji katika jimbo la chalimze
ni mkubwa lakini shule yetu ya mboga imekuwa ni kipaumbele sana kutokana
na mazingira.
Aliongeza
kuwa kutatuliwa kwa changamoto ya maji kutapelekea juongezeka kwa ufaulu kwa
wanafunzi kwani maji yalikuwa yakiumiza vifwa vya watumishi wa shule kutokana
na kuwatuma wanafunzi kwenda sehemu mbalimbali kutafuta maji ili waweze kupata
huduma ya chakula,hivyo maji hayo yatarahisisha shughuli za usimamizi na
uendeshaji wa shule pia ogezeko la ufanisi wa ufundishaji kwa walimu
kutokana na kipindi cha nyuma walimu
walikuwa wakiwazia maji kwa ajili ya matumizi ya familia zao.
Aidha
amemhakikishia mbunge huyo kuwa hakuna yeyote Yule atakayehalibu miundombinu ya
maji hayo kwani si muda mrefu walikuwa wakilia kwa tatizo la kukosa maji hivyo
kila mtu katika eneo hili ni mlinzi wa mwenzake katika mradi huu.
Naye
Mjumbe wa kamati ya bodi ya shule Muhamed Mzimba amempongeza mbunge huyo kwa
kufanikisha lengo lake la kuhakikisha taasisi za serikali zote katika jimbo la
chalinze zinakuwa na visima virefu kwa kusudi la kutatua changamoto za
maji,taasisi hizo ni pamoja na mashuleni,vituo vya afya na sehemu mbalimbali
zenye kutoa huduma za kijamii zinapata visima vya maji.
Aliongeza
kuwa uwepo wa kisima hicho katika shule hiyo kutafanikisha mambo mengi ya shule
kuweza kusonga mbele kutokana na upatikanaji wake.
Kwa
upande wake mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo Juma Ally amempongeza mbunge wa chalinze kwa kuichaingia shule yao misaada mbalimbali
katika harakati zake za kuisaidia
shule yao
No comments:
Post a Comment