NA
MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
MZEE
mmoja aliyetambulika kwa jina la Visu Urembo (80),amefariki dunia baada ya
kuchomwa mkuki kwenye sehemu ya ubavuni mwa mwili wake, katika mgogoro wa
wakulima na wafugaji, uliotokea Lukenge, tarafa ya Ruvu, Kibaha Vijijini, mkoani Pwani.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP, Wankyo Nyigesa
alisema tukio limetokea majira ya saa 12 alasiri, march 26 mwaka huu.
Alieleza,
mzee Urembo kabla ya kufikwa na umauti alikimbizwa kituo cha afya Mlandizi,
ambapo baadae alikimbizwa hospital ya Tumbi kwa matibabu zaidi lakini kabla ya
kupatiwa matibabu madaktari waligundua kuwa umati umeshamfika.
Hata
hivyo, Wankyo alibainisha, wafugaji hao waliingiza mifugo yao (ng’ombe) kwenye
bwawa linalotumika katika shughuli za binadamu ikiwemo kunywa, kufulia, kupikia
na kadhalika.
“Kwa
kuona hivyo ndipo wakulima wakaenda kwa mhemko kuwazuia watoe ng ‘ombe wao
lakini wafugaji walianzisha tafrani, ambapo walianza kurusha mikuki ,vitu
vyenye ncha kali na kusababisha kifo cha mzee huyo na kujeruhi watu watatu
“alifafanua Wankyo.
“Polisi
tulifika eneo la tukio alfajir March 27 ,na kutuliza tafrani hiyo na sasa hali
ni shwarii”.
Wankyo
aliwataja waliojeruhiwa ,kuwa ni pamoja na John Kisukari Urembo (50) ambae ni
mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Lukenge.
Wengine
ni mtendaji wa kijiji cha Lukenge Maximillian Evarist (34) na Adam Onesha ambae
ni mwenyekiti wa kamati ya maji kijijini hapo .
Kamanda
huyo alitoa wito, jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kuepukana na
madhara kama hayo yaliyojitokeza.
Wankyo,alisema
kila mtu katika nchi hii ana haki ya kuishi, kutumia ardhi hii, na hakuna
mwenye mamlaka juu ya mwenzie ila inabidi kuacha kuingiliana mipaka iliyotengwa
kwa ajili ya kundi jingine ili hali kukabiliana na migogoro hasa ya wakulima na
wafugaji”alisisitiza Wankyo.
Mkuu
wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama aliyataka makundi hayo yaheshimiane
na kujenga upendo badala ya kujiona kundi moja ni zaidi ya kundi jingine.
No comments:
Post a Comment