NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
Kamati
ya kudumu ya Bunge , kilimo, mifungo na Maji imeishauri serikali kuharakisha
mchakato wa kuwalipa wakulima wa korosho waliosalia baada ya kumalizika zoezi
la uhakiki febduari 15 mwaka huu ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza
Kauli
ya kamati hiyo ya bunge imetolewa jana katika kikao kilichofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kilichowakutanisha , wakulima
kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara, Waziri na Naibu Waziri wa kilimo, Wakurugenzi
wa Halmashauri, wakuu wa idara kilimo, Mifugo Uvuvi na Maji
Kauli
ya kamati hiyo imekuja baada ya kuibuka maswali kutoka kwa wakulima ya kutaka
kujua ni lini Serikali itawalipa wakulima hao baada ya kumalizika kwa uhakiki
wa zao hilo
Akizungumza
kwa niaba ya kamati hiyo mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Ruvuma
Sikudhani Chikambo alisema kuwa kitendo cha Serikali kuchukuwa muda mrefu bila
ya kuwalipa wakulima kunaweza kuzua migogoro baina ya wakulima na Serikali na
hata kupelekea Wananchi kukosa imani na Serikali yao
“ilipotoka
kauli ya Rais ya kutaka kununua korosho zote kwa sh.3300 bila shaka ilikuwa na
nia mzuri ya kuwasaidia wakulima ila mashaka yangu juu ya jambo lile
inawezekana tumeshindwa katika utekelezaji wa zoezi wakati linafanyika na hiyo
ndio inayosababisha zoezi hili kuchukuwa muda mrefu”
Kauli
hiyo ya chikambo iliugwa mkono pia na Mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa
Dar-es-salaam Lucy mageseli ambapo alisema kuwa hakuona sababu ya wakulima hao
kucheleweshewa fedha zao kwa kuwa Serikali ilishasema kuwa inafedha za kutosha
kuwalipa wakulima ambapo alimtaka Waziri wa Kilimo wakati akijibu maswali
ya wakulima hao awahakikishie kama fedha za kuwalipa wakulima hao zipo ama laa
“Mimi
nashangaa hili swala la uhakiki limetokea wapi? Kwanini misimu iliyopita
haukufanyika? Au kwa sababu msimu huu Serikali ndio imenunua na kama mlisema
tayari fedha mnazo za kutosha kuwalipa wakulima wote kwanini mnachelewa
kuwalipa? mimi nadhani labda mnavutamuda ili kutafuta hiyo fedha ya
kuwalipa wakulima” Alisema Mgeseli
Nae
mbunge wa Shauri moyo Zanzibar Maftar Salim alitumia fulsa hiyo kuishauri
Serikali kuanza maadalizi ya uhakiki kwa wakulima hao mapema wakati wa
kuelekea msimu ujao wa kilimo 2019/2020 ili kuepuka usumbufu uliojitokeza kwa
msimu huu
Wakiongea
kwa masikitiko makubwa mbele ya kamati hiyo ya bunge iliyoambatana na waziri wa
kilimo, wamesema kwa kuwa uhakiki umeshakamilika ni vyema wakaharakisha malipo
yao kwani muda wa kuanza maandalizi ya msimu ujao umeshafika ili wafanye
mapema
Nae
Issa Mkombwe kutoka chama cha msingi Rutamba alisema kuwa kama wakulima
wakubwa wa zao hilo changamoto kubwa wanayokumbana nayo kwa wakati huu ambao
wanasubiri malipo wengi wao wanaishi kwa hofu ya kutaifishwa mali zao
kutokana na kuchelewa kwa marejesho ya mikopo yao katika taasisi mbali mbali za
kifedha lakini hata kwa vibarua wadogo wadogo ambao waliwatuma kupalilia
mikorosho yao pamoja na wakati wa kuokota korosho ambapo walitakiwa kulipwa
baada ya kupata fedha hizo
“
kabla ya kuingia katika dhahama hii mimi sikuwahi kuugua presha lakini toka
mwezi januari nimegundulika nina presha ya kushuka kama unataka waziri hata
vyeti ninavyo hii ni kutokana na mawazo niliyonayo kwanza nadaiwa kiasi kikubwa
na Bank na deni hilo linazidi kukua siku hadi siku, lakini mbaya zaidi
nanyimika raha usiku silali vizuri kila siku hodihodi za wale vibalua
walionisaidia kuokota korosho wakitaka niwalipe ela zao mimi nazitoa wapi?
Mtatuuwa wenzenu” alisema mzee huyo
Kufuatia
hatua hiyo waziri wa kilimo Japhet Hasunga ameahidi kuwalipa wakulima hao
waliosalia huku akiwapa wiki mbili bodi ya mazao mchanganyiko pamoja na benki
ya maendeleo ya kilimo TADB kuhakikisha malipo hayo yanakamilika kwa
wakati
No comments:
Post a Comment