Mtendaji Mkuu wa TFS Profesa
Dos Sontos Silayo akiangalia mitambo ya kuchakata asali iliyofungwa wilayani
Manyoni mkoani Singida.
Mitambo ya kuchakata asali
ambayo imefungwa katika kiwanda cha TFS wilayani Manyoni,mkoani Singida
.........................
WAKALA wa
Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umefunga mtambo wa kuchakata asali wilayani
Manyoni mkoani Singida.
Akizungumza
leo Machi 14,2019 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TFS Tulizo Kilaga amesema
mtambo huo wa kisasa una uwezo wa kuchakata lita 500 kwa siku.
Amesema
kuwa mtambo huo umegharimu Sh.milioni 80 na unatarajiwa kuondoa changamoto ya
uwepo wa asali yenye kiwango duni cha ubora katika ukanda huo na maeneo maeneo
ya jirani.
“Mtambo huu
umefungwa katika kiwanda cha TFS na utatumiwa na wafugaji wa nyuki wa ndani
pamoja na nje wote wataruhusiwa kuchakata mazao yao,”amesema Kilaga.
Ameongeza
kuwa kiwanda hiko kwa kiasi kikubwa kitategemea mali ghafi toka kwenye msitu wa
Aghondi uliopo eneo la Itigi na uwepo wa mtambo
huo pia utasaidia kutunza mazingira kwani watakuwa na uhakika wa soko la asali
yao.
Pia amesema
katika uvunaji wa awali wamefanikiwa kuvuna mizinga 459 kati ya 729 na kupata
asali kilo 6,175 sawa na tani 6.175 wastani kilo 13.45 kwa mzinga.
Akizungumzia
mtambo huo, Meneja wa TFS wilayani Manyoni Juma Mambo amesema utasaidia
kupatikana kwa asali bora na hivyo kuwa na uhakika wa soko la ndani na nje
ambalo litawafanya wadau kujiongezea kipato.
No comments:
Post a Comment