Mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)
akisisitiza umuhimu wa mbegu bora za kilimo wakati akizungumza kwenye
hafla ya uzinduzi wa Mpango wa kuimarisha Mitandao ya Usambazaji wa Mbegu na
Viuatilifu, katika ukumbi wa Usungilo Hoteli Jijini Mbeya, Tarehe 5 Machi
2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
..........................
Na Mathias
Canal, Wizara ya Kilimo-Mbeya
Uimarishaji
wa mitandao ya usambazaji mbegu na viuatilifu ni muhimu katika kuhakikisha tija
inaongezeka katika Uzalishaji wa mazao yote hususani nafaka, matunda mbogamboga
na mbegu za mafuta.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 5 Machi 2019 wakati
akizindua Mpango wa kuimarisha Mitandao ya Usambazaji wa Mbegu na Viuatilifu,
Mpango unaotekelezwa na Mradi wa NAFAKA na Kampuni ya Kimataifa ya CORTEVA
katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini nchini Tanzania.
Katika
hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Usungilo Hoteli Jijini Mbeya Mhe
Hasunga alisema kuwa kuimarisha usambazaji mbegu na viuatilifu utamsaidia mkulima
kuwa na uhakika wa chakula na kuongeza pato lake hivyo kuchangia katika
kuipeleka Tanzania kufikia Uchumi wa Kati kama inavyoeleza sera ya Serikali ya
awamu ya tano inayongozwa na Mhe Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Alisema
wakulima nchini Tanzania wanategemea Sekta ya kilimo kuchangia katika ukuaji wa
uchumi na maendeleo ya wananchi, kwa kuwa inatoa ajira kwa asilimia 65 ya
wananchi, ina uwezo wa kutoa malighafi ya viwanda kwa asilimia 66 na inachangia
asilimia 100 ya chakula kinachopatikana.
Alisema
kwa kuzingatia umuhimu wa sekta hiyo, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa
maendeleo inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo awamu ya II
yaani Agricultural Sector Development Program – ASDP II inaolenga
kuleta Mapinduzi katika sekta ya kilimo.
Programu
hiyo ya miaka kumi (10) imeanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2018 na inafanyia
kazi maeneo ya Usimamizi endelevu wa ardhi na maji, Kuongeza Tija (kuongeza
matumizi ya pembejeo), Kuongeza masoko na kuongeza thamani ya mazao, Kuboresha
mazingira ya uwekezaji katika kilimo. Hivyo, Uimarishaji wa Mpango wa Kusambaza
Pembejeo na Viuatilifu ni moja ya shughuli muhimu katika Program ya Kuendeleza
Sekta ya Kilimo -ASDP 11 katika kuongeza tija.
“Ni
Imani yangu kuwa, kufanikiwa kwa kazi hii ya Mradi wa Nafaka ni kufanikiwa
katika utekelezaji wa sehemu ya Programu ya Kuendeleza Kilimo nchini ASDP II.
Mradi huu pia utaendelea kuimarisha mahusiano yaliyopo baina na Serikali na
Sekta nafsi katika kuendeleza kilimo nchini” Alisema
Kadhalika,
Hasunga alisema Serikali inatambua mchango unaotolewa na Shirika la
Misaada la Marekani USAID katika miradi mbalimbali husasani katika sekta ya
kilimo. Mradi wa NAFAKA ni moja ya michango ya Shirika la USAID katika kuongeza
tija kupitia Mashamba darasa, Uendeshaji wa Vikundi na vyama vya wakulima,
Kuongeza thamani kwenye usindikaji wa Mahindi kwa njia ya virutubishi kwenye
unga, Kuunganisha wakulima na huduma za kifedha Masoko na Bima ya Mazao
yaani “Crop Insurance”.
Alisema
kuwa Shughuli hizo zinazotekelezwa na Mradi wa NAFAKA kwa kushirikiana na
CORTEVA unaenda sambamba na jitihada za Wizara ya Kilimo katika
kuendeleza kilimo. Moja ya maeneo ya kipaumbele yanayotekelezwa na Wizara ni
kuongeza tija katika uzalishaji kwa kuimarisha upatikanaji wa pembejeo, na
kuimarisha huduma za ugani.
Maeneo
mengine ya Kipaumbele ya Wizara ya Kilimo ni Kutungwa kwa sheria ya kilimo ili
kusimamia kilimo, Kuandikisha wakulima wote, Kuongeza uzalishaji wa sukari
kuondoa upungufu wa sukari nchini, Kufungamanisha uzalishaji na mahitaji ya
viwanda ili kutoa mali ghafi ya viwanda kwa kuongeza uzalishaji, Kuongeza
uzalishaji wa mazao ya mafuta, Kuanzisha scheme za umwagiliaji ili kuongeza
eneo la kilimo cha umwagiliaji, Wakulima kuwa na bima ya mazao, na Kuongeza
fursa za upatakanaji wa fedha kwa wakulima.
“Ni
jambo la faraja kuona sekta binafsi sasa zinatoa mchango katika jitihada za
Serikali katika kutoa mafunzo kwa wakulima kwa kuanzisha mashamba darasa, kutoa
mafunzo kwa maafisa ugani, kusimamia na kuhimiza matumizi ya mbegu bora na
viuatilifu pamoja na kufanya kazi na mawakala wa pembejeo wa daraja la kati na
wadogo waliopo vijijini wapatao” Alikariirwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa.
“Ni
jambo la kutia moyo kuwa mpango huu utasaidia usambazaji na upatikanaji wa
viuatilifu vya kupambana na visumbufu vya mlipuko vikiwemo viwavi jeshi vamizi
“Fall Army Worms” katika maeneo yaliyovamiwa kwenye Mikoa ya Nyanda za Juu
Kusini nchini mwetu”
Aidha,
alisema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika kilimo
ikiwa ni pamoja na kufanya mapitio katika taratibu zilizowekwa katika
uzalishaji, usambazaji na uingizaji wa mbegu ili kurahisisha upatikanaji wa
mbegu bora kwa wakulima nchini.
Katika
suala la soko la mahindi Serikali imesharekebisha suala hil0 na itaendelea kutoa
taarifa za hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha taratibu za
masoko ya mazao ili wakulima, wafanyabiashara na wadau waweze kunufaika na
uwekezaji katika sekta ya kilimo.
Sambamba
na hayo pia Waziri Hasunga alisema kuwa serikali itaweka msisitizo katika sekta
ndogo ya ardhi ili wakulima kuona umuhimu wake na kuondokana na kilimo
kinachotegemea mvua.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)
akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Mpango wa kuimarisha Mitandao ya
Usambazaji wa Mbegu na Viuatilifu, katika ukumbi wa Usungilo Hoteli Jijini
Mbeya, Tarehe 5 Machi 2019.
Sehemu ya washiriki wa uzinduzi wa Mpango wa kuimarisha
Mitandao ya Usambazaji wa Mbegu na Viuatilifu katika ukumbi wa Usungilo
Hoteli Jijini Mbeya wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) Tarehe 5 Machi 2019.
Sehemu ya washiriki wa uzinduzi wa Mpango wa kuimarisha
Mitandao ya Usambazaji wa Mbegu na Viuatilifu katika ukumbi wa Usungilo
Hoteli Jijini Mbeya wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) Tarehe 5 Machi 2019.
No comments:
Post a Comment