Mkurugenzi wa Huduma
za Misitu Emanuel Wilfred (aliyesimama) akiwasisitizia watumishi wa
TFS makao makuu (hawapo pichani) kufanya kazi kwa weredi kwenye utekelezaji wa
majukumu yao leo 7 Februari 2019. Aliyekaa ni Mkurugenzi wa Rasilimali Misitu,
Zawadi Mbwambo akifuatilia mkutano huo.
............................................
Mkurugenzi wa Huduma
za Misitu Emanuel Wilfred (pichani) amewataka watumishi wa Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na kwa
kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma na kujiepusha na
kutenda kinyume kwenye utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza katika mkutano na
wafanyakazi wa amakao makuu ya TFS jijini Dar es Salaam mapema hivi leo,
Wilfred amesema TFS katika kutekeleza majukumu yake ya msingi ya
kuhakikisha inasimamia rasilimali za misitu ili zisaidie katika
uchumi wa taifa kwa kizazi cha sasa na kijacho, imebaini kuwepo kwa
ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu miongoni mwa watumishi wake.
Amesema katika siku za hivi karibuni
kumeibuka wimbi kubwa la watumishi wenye utendaji usioridhisha na wanaokiuka
maadili ya utumishi wa umma waliopo makao makuu na hata mikoani.
“Sijawahi shuhudia watumishi wengi
wakichukuliwa hatua za nidhamu kama mwaka huu. Watu wanafanya mambo
yasiyovumilika yani utakuta mtumishi anatoweka tu kazini bila kutoa taarifa
wala kuomba ruhusa! Mtumishi kutokuwepo kazini kwa siku tano bila ruhusa wala
sababu za msingi adhabu yake ni kufukuzwa kazi. Sasa nawatangazia mtumishi yoyote
atakayekosekana katika kituo chake cha kazi huku mwajiri wake hajui,
atachukuliwa hatua.” Amesema.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo aliwataka
watumishi ambao hawajaenda kwenye mafunzo ya Jeshi Usu kujiandaa kisaikologia
kutokana na TFS kubadiri rasmi muundo wake na kuwa Jeshi Usu ambapo tayari
watumiashi wa makao makuu wameanza utekelezaji wake.
Aidha, Mkurugenzi huyo aliwaeleza
watumishi hao kuwa sambamba na mabadiriko hayo kuna marekebisho ya mishahara
yanayoendelea ambapo tayari kuna baadhi wamepata mshahara mpya huku wengine
wakiendelea kuhakikiwa ili wapate mshahara huo.
“Watu msiwe na wasiswasi najua
wengine mshapata mishahara mipya huku wengine wakiwa hawajapata, waendelee kuwa
wavumilivu taratibu za uhakiki zinaendelea na kwa miezi ambayo itakuwa
hamjapata mtajaza fomu za madai ili kupata haki yenu,” alisema Mkurugenzi.
No comments:
Post a Comment