MAKAMU wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amewataka
wafanyabiashara wadogo kulipia na kuchukua vitambulisho maalumu vilivyotolewa
na Serikali kwa ajili yao vinginevyo vitahesabika kuwa ni wafanyabiashara
wakubwa wanaopaswa kulipia kodi.
Hatua
itasaidia kuwatambua na kuepusha usumbufu wakati wa kufanya shughuli zao za
kujiletea maendeleo.
Makamu wa
Rais alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa TASAF
wilayani Sikonge ikiwa ni siku tatu ya ziara yake mkoani Tabora.
Alisema
mfanyabiashara ndogo ndogo asiyetaka kulipia shilingi 20,000/- za kitambulisho
maalumu atahesabika kuwa yeye anapaswa kukata leseni na kulipa kodi kama
walivyo wafanyabiashara wakubwa.
Makamu wa
Rais aliongeza kuwa kama shilingi 20,000/- zinaonekana ni nyingi kwa baadhi ya
wafanyabiashara wadogo kulipa kwa mkupuo, uongozi wa Mkoa, Wilaya unaweza
kuweka utaratibu ambao utawawezesha kulipa kwa awamu.
Alisema
mfanyabiashara huyo anaweza kulipa kwa awamu mbili au tatu na akishamaliza
malipo anakabidhiwa kitambulisho chake.
Aidha
Makamu wa Rais alitoa angalizo kwa viongozi wa Mamlaka ya Mikoa na Serikali za
Mitaa kuhakikisha hakuna Mfanyabiashara atakayepewa kitambulisho kabla ya
kumaliza malipo yote kuwa upo uwezekano wa kutoroka na kwenda Mkoa mwingine na
kuendesha shughuli zake kwa kutumia kitambulisho ambacho bado anadaiwa.
No comments:
Post a Comment