Na
Hadija Hassan, Lindi
Baraza
la Aridhi Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi linakabiliwa na changamoto ya kukosa
Mwenyekiti wa kudumu kwa zaidi ya miaka mitatu hali inayopelekea
kuchelewa kumaliza mashauri kwa wakati
Hayo
yameelezwa na kaimu mwenyekiti wa Baraza hilo Saidi Wambili jana
alipokuwa anazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG wakati maazimisho ya wiki ya sheria Nchini
yaliyofanyika katika viwanja vya Ilulu Manispaa ya Lindi Mkoani humo
Wambili
alisema changamotokubwa inayoikabili Baraza hilo kwa sasa ni kukosekana kwa
mwenyekiti wa kudumu hali inayopelekea kuchelewa kumalizika kwa baadhi ya
mashauri yanayofika katika baraza hilo
“baraza
la Aridhi Lindi kwa kipindi cha miaka mitatu halina mwenyekiti wa kudumu mimi
ni mwenyekiti wa baraza la Aridhi la mtwara hivyo nalazimika kufanya kazi kwa
maeneo yote mawili hiyo wakati mwingine namna ya kujigawa inakuwa ni
vigumu hivyo hiyo changamoto ni kubwa na ninyeti sana”
alieleza Wambili
Aliongezakuwa
licha ya baraza hilo kukosa mwenyekiti wa kudumu pia baraza hilo linakabiliwa
na changamoto ya watumishi 5 kwani aliyopo kwa sasa ni mtumishi
mmoja wa kada ya ukalani pekee
Alisema
hali hiyo pia inamfanya kalani huyo kufanya kazi nyingine ambazo sio za kwake
kama vile kupokea na kupeleka mashauri mahakamani, kupokea Ada za mahakama
pamoja na shughuli za kiutawala
Alisema
ili kuwe na mgawanyo mzuri wa kazi kwa mujibu wa ikama ya watumishi
Baraza hilo lilikuwa linahitaji watumishi 6
Wambili
aliongeza Baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo limekuwa likipokea
mashauri yasiyopungua 160 yanayohusu Rufaa, Maombi madogo mashauri ya
kutekelezakwa hukumu,
No comments:
Post a Comment