Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akipokea daftari la mama aliyemleta mwanae kupata huduma katika
Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, wakati akiwa katika ziara
yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo. Wakatikati
ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Lobikieki Kissambu.
...................................
Na WAMJW –
MTWARA
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile amewaasa watumishi wa wekta ya afya nchini kuacha tabia ya kufanya
kazi kwa mazoea, na wajikite katika kutoa huduma kulingana na sheria na
taratibu za taaluma zao.
Ameyasema
hayo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya kwa
wananchi katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara – Ligula.
Katika
ziara hiyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa licha ya jitihada za kuboresha huduma za
afya kwa wananchi, ni wajibu wa kila mtoa huduma za afya nchini kuhakikisha
anatimiza wajibu wake bila shurti na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
“Nyinyi
mnafanya kazi kwa mazoea, kwa nini hamjajaza taarifa wala kusaini katika fomu
ya wagonjwa, na hili linaendana na maelekezo ambayo Serikali tunawapa, kwamba
kila mtu aandike tarehe na muda ambao amefanya kazi, nyinyi maabara hamfanyi”
alisema Dkt. Ndugulile
Pia, Dkt.
Ndugulile amesema kuwa Serikali imeboresha vituo vya afya zaidi ya 300, ambavyo
vitatoa huduma za dharura za upasuaji wakumtoa mtoto tumboni, na hospitali za
wilaya 67, katika Mkoa wa Mtwara hospitali za wilaya 3 zinaenda kujengwa, ili
kupunguza mzigo katika hospitali za mikoa,
Aidha, DKt.
Ndugulile amesema kuwa amesema kuwa kutokana na Hospitali hiyo kuwa na
Changamoto za x-ray na gari la kubebea Wagonjwa, Serikali imeahidi kuzitatua
changamoto hizo kwa muda mfupi ili wananchi wa Mtwara waanze kupata huduma hizo
mara moja.
“Mmeongelea
huduma za mionzi (x-ray), niwaahidi tutawaletea mashine mpya ya x-ray za
kidigitali, lakini vile vile kama kuna changamoto ya gari la kubebea wagonjwa,
zikija tutazigawa, tunataka hospitali za mikoa zianze kuonekana kwamba ni
hospitali za mikoa kweli” alisema Dkt. Ndugulile
Mbali na
hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali inatambua pengo la watumishi katika
sekta ya afya, hivyo mwaka uliopita iliweza kuajiri watumishi takribani
11,000, huku watumishi 3000 kuziba pengo la watumishi ambao hawakuwa na vigezo,
na 8000 walikuwa ni ajira mpya.
“Tumeweza
kuajiri Watumishi takribani 11,000, 3000 kuziba pengo la watumishi ambao
hawakuwa na vigezo na vyeti, na ajira mpya ni 8000, kuwahiyo jumla watumishi
11, kadri tunavoendelea kupata uwezo tutaendelea kuongeza rasilimali watu
kuhakikisha kwamba tunaziba mapengo yaliyopo” alisema DKt. Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua mkoba wa Vifaa vya
kujifungulia, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya
katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua
Kadi inayoonesha Idadi ya Dawa katika Chumba cha dawa, wakati akiwa katika
ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya
Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Idadi ya
Wagonjwa waliosajiliwa kwenye mfumo, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua
hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara
Ligula.
No comments:
Post a Comment