Na
HADIJA HASSAN, LINDI.
Kutokana
na tatizo la mimba kwa watoto wa kike wa Mkoa wa Lindi kuwa kumbwa, Mkoa
huo umezindua kampeni maalumu ya kupinga mimba za utotoni
ambayo inajulikana kwa jina la “msaidie ,akue,asome Mimba Baadae
Uzinduzi
huo ulifanyika February 9 mwaka katika Viwanja vya shule ya Msingi Mpilipili
katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi uliambatana na maandamano ya wanafunzi
kutoka katika shule mbali mbali za msingi na sekondari za manispaa hiyo
yaliyongozwa na wanawake viongozi waliofanikiwa wa Mkoa huo,
Katika
Maandamano hayo baadhi ya wanafunzi hao walionekana wakibeba mabango
yenye ujumbe unaosomeka “niache nisome mimba baadae, mzazi /mlezi
nitunze nitimize ndoto zangu nataka shule sio mimba , miba baadae.
Mambango
mengine yalikuwa yakisomeka “Vyukuvyuku hata kwetu vipo, nifanye kama mwanao
nami nina ndoto, huoni hata aibu tafuta saizi yako, kuitwa nanunu mimi
bado pamoja na niite dada hayo yote yakiwalenga wanaume wenye tabia
ya kuwaraghai mabiti wadogo kimapenzi na hatimae kuwapa ujauzito
Akitoa
Taarifa ya kampeni hiyo Katibu Tawala wa Mkoa Huo Bi, Rehema Madenge
alisema kuwa Lengo kuu la Kampeni
hiyo ni kuimarisha mifumo ya ulinzi kwa Watoto kuanzia ngazi ya kaya hadi mkoa
kwa kuwajengea uwezo wataalamu wanaoshughulikia masuala ya ulinzi na usalama wa
watoto
Kutoa
Huduma kwa wahanga wa mimba za Utotoni ambapo huduma endelevu kwa
watoto waliopata mimba na kuhakikisha Afya bora kwa watoto watakao zaliwa ikiwa
ni pamoja na ufuatiliaji wa mashauri ya watoto na kuwapatia msaada wa
kisaikolojia watoto waliopata mimba
Alitaja
lengo linguine la kampeni hiyo kuwa ni kusimamia na kuchukuwa hatua za makusudi
katika kuzuia mimba za utotoni kwa kufanya mikutano ya kutoa elimu na
kuwajengea uwezo watoto, wazazi, walezi na wadau juu ya madhara ya mimba za
utotoni kwa kuhusisha vyombo vya habari na kutumia elimu ya sanaa
Madenge
alisema katika Mkoa huo ongezeko la mimba za utotoni linauhusiano mkuwa na
malezi duni ya wazazi ama walezi ambapo wazazi wengi wa maeneo hayo hawako
makini katika kufuatilia malezi na makuzi ya watoto wao.
Hata
hivyo madenge alisema kuwa jambo hilo uwafanya watoto hao kuwa huru, kufanya
wanachokitaka, kucheza katika mazingira hatarishi ambako wanakuwa wanajifunza
mambo mengi yasiyostahili kwa umri wao.
“ukiangalia
kwa kiasi kikubwa jambo hili upelekea kumomonyoka kwa maadili, na mwisho wake
watoto hawa upata mimba wakiwa katika umri mdogo” alifafanua Madenge
Akizindua
kampeni hiyo Mkuu wa Mkoa Lindi, Godfrey Zambi ameziagiza shule zote za Msingi
na Sekondari za Mkoa huo kujiwekea utaratibu wa kuwapima mimba wanafunzi mara
tatu kwa mwaka , pamoja na kumtaka Mganga Mkuu wa Mkoa huo kuhakikisha anakuwa
na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kutekeleza agizo hilo
Hata
hivyo Zambi aliagiza kuchukuliwa kwa hatua kali ikiwa pamoja na kuwaweka ndani
wazazi wa watoto wa alieweka na aliewekwa mimba pamoja na kijana wa kiume ili
kutoa fundisho kwa wazazi wasiowalea vyema watoto wao pamoja na vijana
wenyetabia ya kuwataka kimapenzi watoto wadogo
Nae
katibu tawala msaidizi utawala rasilimali watu wa mkoa huo DKT, Bora Haule
aliyataja baadhi ya matarajio ya kampeni hiyo kuwa ni kuisha kabisa kwa tatizo
hilo la mimba kutokana na kuimarika kwa mifumo ya ulinzi na usalama wa
mtoto,kuongezeka kwa uwezo wa jamii katika kusimamia na kuchukua hatua kuzuia
mimba za utotoni.
Mengine
ni wadau wote kushiriki katika vita juu ya kutokomeza mimba za utotoni , kuwepo
na ufahamu juu ya athari za mimba za utotoni kwa wanajamii wa lindi pamoja na
huduma za Afya kutolewabila kikwazo kwa watoto wote walopata mimba na watoto
waliowazaa
Hayo
ni baadhi ya mabango yaliyobebwa na wanafunzi kama yanavyoonekana yakiwa na
ujumbe wa aina mbalimbali unaopinga mimba katika umri mdogo kwa wanafunzi.
Hayo
ni baadhi ya mabango yaliyobebwa na wanafunzi kama yanavyoonekana yakiwa na
ujumbe wa aina mbalimbali unaopinga mimba katika umri mdogo kwa wanafunzi.
No comments:
Post a Comment