Mbunge wa malindi Mhe Ally Saleh Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wabunge wa chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaamna, KULIA ni mbunge wa jimbo la mchinga Mhe Hamidu Bobali. wameiomba mahakama kutolea huku shauri lao. |
Na Selemani Magali
"Kwa heshima na taadhima tunamuomba Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi
waliangalie suala hili kwa umuhimu na uzito maalumu kwa sababu kuchelewa
kwake kunakiathiri chama chetu kwa kiasi kikubwa," ni Kauli ya Mbunge wa Malindi Bw. Ally Saleh wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuiomba Mahakama kutoa hukumu ya shauri lao
namba 23/2016 linalohusu uhalali wa uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba
kwa chama CUF.
Ally amesema kuna athari kubwa wanazipata toka kesi hiyo kufikishwa mahakamani na kwamba waathirika wakubwa ni wabunge lakini pia inawagharimu rasilimali fedha, muda na kuibiwa ruzuku zaidi ya
Sh1.5 bilioni na uharibifu wa mali za chama zikiwamo magari na majengo.
.
"Chama kinashindwa kuendesha shughuli kwa utulivu na kujiandaa na
chaguzi za ndani na za kiserikali kwa mwaka huu 2019 na uchaguzi mkuu
2020" amesema Saleh.
Naye Bobali amesema athari anazopata ni kubwa ikiwamo kutofanya siasa kwa kipindi chote tangu mgogoro huo ulipoanza.
Bobali ambaye pia ni mwenyekiti wa vijana wa chama hicho amesema mgogoro
huo unawatoa kwenye ushindani wa kisiasa kwa sababu unawaweka mbali na
wanachama wao na majimbo yao kwa ujumla.
"Tunashindwa kufanya siasa, kwa sababu baadhi ya maeneo wenyeviti wa
chama kwa eneo husika wanakuwa upande wa Lipumba na sisi tupo upande
halali wa Maalim Seif, huu mkanganyiko unatusukuma kuiomba mahakama
kutoa hukumu ya kesi hiyo ili tuendelee na majukumu yetu angalau kwa
kipindi hiki kifupi kabla ya uchaguzi mkuu 2020," amelalama Bobali.
Februari 22, 2019 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilisogeza mbele
utoaji hukumu ya mgogoro wa uongozi ndani ya CUF na sasa hukumu hiyo
itatolewa Machi 17, 2019.
No comments:
Post a Comment