Mnamo
tarehe 11.02.2019 majira ya saa 23:45 usiku huko eneo la Soweto, Kata ya
Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
lilikamata gari lenye namba za usajili T.937 CKD aina Toyota Saloon likiwa na
vipodozi vya aina mbalimbali vilivyopigwa marufuku nchini. Vipodozi
vilivyokamatwa ni:-
1.
Extra
Clair katoni nane [08].
2.
Perfect
White katoni mbili [02].
3.
Epiderm
Cream dazani arobaini na saba [47]
4.
Diproson
dazani ishirini na moja [21]
5.
Coco Pulp
katoni mbili [02]
6.
Carolight
katoni sita [06]
7.
Citro
Light katoni tatu [03]
8.
Teint
Clair katoni mbili [02]
9.
Top Lemon
katoni nne [04]
10.
Clair Men
katoni mbili [02]
11.
Princes
Clair katoni nne [04]
12.
Movet
boksi mbili [02]
13.
Miki Clair
katoni mbili [02]
14.
Top Clair
Plus katoni moja [01]
15.
Collagen
formula boksi mbili [02]
16.
Mont Clair
boksi mbili [02]
17.
Movet tube
pcs mbili [02]
18.
Movet
boksi mbili [02]
19.
Cocoderm
boksi moja [01]
KUPATIKANA
NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU NCHINI.
Mnamo
tarehe 12.02.2019 majira ya saa 07:15 asubuhi huko eneo la Check Point Igurusi,
Kata ya Igurusi, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali na Mkoa wa Mbeya, Polisi
wakiwa doria walimkamata SAID IDDY @ MOHAMED [32] Dereva na Mkazi wa Mbadula
Arusha akiendesha gari lenye namba za usajili T.298 DCH aina ya Scania Basi la
abiria – HAJI’s akitokea Mbeya kuelekea Arusha akiwa na vipodozi vilivyopigwa
marufuku nchini aina mbalimbali.
Vipodozi
vilivyokamatwa ni:-
1.
Diana
Boksi mbili [02].
2.
White Max
Boksi tatu [03].
3.
Secret
White Location Boksi moja [01]
Upelelezi
unaendelea na mara baada ya kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.
KUPATIKANA
NA SILAHA [GOBORE] BILA KIBALI.
Mnamo
tarehe 11.02.2019 majira ya saa 14:35 mchana huko eneo la Makasini – Uyole,
Kata ya Uyole, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi
walimkamata PAUL ABRICK [66] Mkazi wa Mtaa wa Nyahoro – Uyole akiwa na silaha
Gobore aina ya Tower yenye namba 1878 bila kibali. Upelelezi unaendelea.
No comments:
Post a Comment