Mgeni katika shughuli hiyo, Mkuu wa Dawati la kijinsia kutoka makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, DCP Maria Nzuki akielezea jambo katika Kampeni hiyo. |
Mkurugenzi mtendaji Lilian Liundii akifafanua jambo |
Mkurugenzi akiiwa na mgeni rasmi katika kampenii hiyo. |
Na Selemani Magali
Kampeni
ya ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili wa kingono- “1-5-5 namlinda” yenye kauli
mbiu “mlinde mtoto afurahie utoto wake,
ujana wake na uzee wake” imezinduliwa jana huku viongozi
wa kidini na jamii kwa ujumla wakitakiwa kutumia majukwaa yao kuhubri juu ya
umuhimu wa kuwalinda watoto dhidi ya vitendo viovu vya ukatili wa kingono,
ikisisitizwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuwalinda watoto.
Akizungumza
katika ufunguzi wa Kampeni hiyo iliyolenga kuamsha Jamii kushiriki katika
kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vyote vya Kingono, Mkuu wa Dawati la
kijinsia kutoka makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, DCP Maria
Nzuki amesema viongozi wa dinii wanayo nafasi ya kupunguza ukatili huo.
“Viongozi wa kiroho wanayo nafasi ya
kutokomeza ukatili wa kingono, wao wanawatu wengi na wanaaminika, wakisema
jambo waumini wao watalipokea na kulifanyia kazi…basi chukueni na hili
mkalifanyie kazi, mara nyingi watu hupendwa kukumbushwa kumbushwa…kumbusheni basi
na hili huwenda kukawa na manufaa.” Aliongeza DCP Nzuki.
Aidha
DCP Nzuki amewaomba jamii kuwalinda watoto kwa kutoa taarifa mapema mara tu
waonapo ona viashiria vya ukatili wa Kingono, ikiwamo watoto wa shule kuingia
quest, kulala katika chumba au nyumba ya msela kisha wakakaa muda mrefu, na
matendo yanayofanana na hayo.
Akielezea hali ya ukatilii wa Kingono
Tanzania DCP Nzuki amesema kumekuwa na ongezeko ambapo sasa kila sehemu ya
yenye wanawake watatu mmoja tayali amewahi kufanyiwa vitendo hivyo, na kuongeza
kuwa tatizo ni kubwa linalohitaji nguvu ya pamoja kuliondoa.
Akizungumzia
hatua mbalimbali zinazochukuliiiiwa na Serikali kupambana na hali hiyo, DCP
Nzuki amesema kwa upande wa Serikali
kupitia Jeshi la polisi tayari jitihada mbali mbali zinachukuliwa
ikiwamo kuweka madawati ya kijinsia katika vituo vya polisi, kuweka vituo vya
mkono kwa mkono katika baadhi ya hosptali (one stop centers) pamoja na kuongeza
usiri kwa watoa taarifa.
Aidha DCP nzuki amewaka wazazi na
walezi wa watoto kufahamu kuwa jukumu la kumlea mototo ni la kwao na wanapaswa
kuhakikisha wanamlinda mototo na vitendo vyote vya ukatili wa kingono.
Amesema wazazi wanajukumu la kuwa
karibu na watoto wao na kuzungumza madhara ya ukatili wa kingono ambapo
itawasaidia watoto kutoa taarifa wakati wanapofanyiwa vitendo hivyo na
watu wasio julikana.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi akielezea kampenii
hiyo, amesema Kampeni hii imelenga kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya athari
za ukatili wa kingono kwa watoto na umuhimu wa kuwalinda dhidi aina hiyo ya
ukatili, kutathmini na kuibua mijadala katika jamii juu ya hali halisi ya
ukatili wa kingono, kuhamasisha jamii kuzuia vitendo hivi visitokee na kutoa
taarifa mara waonapo matukio hayo ya
ukatili wa kingono kwa watoto ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua stahiki.
Amesema Vitendo
hivi vinarudisha nyuma maendeleo ya mtoto na taifa kwa ujumla. Miongoni mwa
athari zitokanazo na ukatili wa kingono dhidi ya watoto ni pamoja na watoto
kuathirika kisaikolojia, maambukizi ya magonjwa ya zinaa na UKIMWI, mimba za utotoni,
na kubwa zaidi ni kuhatarisha ustawi wa taifa na kuchochea uongezeko la vitendo
hivi katika jamii.
Ukatili
wa Kingono Tanzania bado ni tatiizo sugu, kwa mujibu wa tafitii inaoonyesha
kuwa mnamo mwaka 2011, katika wasichana watatu mmoja amefanyiwa na mmoja kati
ya wavulana saba wamekutana na ukatili wa kingono kabla ya kutimiza miaka 18.
Hata hivyo, kulingana na utafiti huo, wengi wa
watoto hawatoi taarifa juu ya vitendo hivyo,
wachache wanatafuta huduma na wachache
zaidi wanafanikiwa kupata matibabu au msaada wanapotoa taarifa ya matukio hayo.
Pia, ripoti iliyotolewa na Kituo cha sheria na
haki za binadamu (LHRC) zinaonyesha kuwa matukio ya ukatili wa kingono miongoni
mwa watoto yanaongezeka nchini.
Kulingana na ripoti hiyo iliyotolewa Juni
2018, wastani wa watoto 394 wamebakwa kila mwezi katika maeneo mbalimbali Tanzania
bara, huku ulawiti wa watoto ukiongezeka kutoka matukio 12 kwa kipindi cha Januari hadi Juni
2017 hadi matukio 533 kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2018, na mikoa inayoongoza
kwa matukio hayo ni Dar es salaam na Iringa.
Ends
No comments:
Post a Comment