Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimjulia hali mama aliyetoka
kujifungua, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya
katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
..................................
NA WAMJW – PWANI
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameziagiza Hospitali za rufaa zote
nchini kuwa na ICU kwaajili ya watoto wachanga ili kupunguza vifo vifo vyao.
Waziri Ummy amesema hayo wakati wa
ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali teule
ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Waziri Ummy ameagiza hayo
kupitia kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo kuwa ahakikishe watoto wachanga
lazima wawe na ICU yao ili kuhakikisha vifo vya Watoto wachanga vinapungua nchini.
“Watoto wachanga wagonjwa, wawe na
ICU yao, lengo letu kama Serikali ni kupunguza Vifo vya Watoto wachanga,
kwasababu tukipunguza vifo vya Watoto wachanga, tutakuwa tumepunguza vifo vya
Watoto wanye umri wa chini ya miaka mitano” alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa
karibu 40% ya vifo vya watoto ni watoto wachanga na katika kila Watoto 100,
Watoto 40% ni Wachanga, hivyo Serikali inaendelea kuchukua jitihada za makusudi
ili kupunguza vifo hivi, ikiwemo kusisitiza kila Hospitali nchini kuwa na ICU.
“Karibu 40% ya vifo vya watoto ni
watoto wachanga na katika kila Watoto 100, Watoto 40% ni Wachanga, kwahiyo
Daktari ni lazima tulifanyie kazi agizo hilo” alisema Waziri Ummy.
Licha ya changamoto alizokutana nazo
Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inatarajia kujenga jengo mahususi kwaajili ya
huduma za Dharura katika Hospitali zote za Rufaa za Mikoa nchini ili kuokoa
maisha ya wagonjwa, hasa waliopata ajali.
“Nafurahi kusema, Serikali imeahapata
fedha kwahiyo tutakuwa na jengo mahususi kwaajili ya huduma za Dharura na
wagonjwa wa ajali, na hii tunataka iwe katika Hospitali za Rufaa za Mikoa zote
ili mgonjwa aweze kuokolewa maisha muda mfupi anapofika Hospitali” alisema
Waziri Ummy.
Pia, Waziri Ummy ameridhishwa kwa
kiasi kikubwa juu ya hali ya upatikanaji wa dawa nchini, huku akiwatoa hofu
Mwananchi kuwa Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ina dawa zakutosha.
Aliendelea kusema kuwa Serikali
imeainisha fani nane nane za kipaumbele ili kuwa na madaktari Bingwa wawili
katika kila fani ikiwemo, Daktari Bingwa wa Watoto, Daktari Bingwa wa magonjwa
yakina mama na uzazi, Daktari Bingwa wa upasuaji wajumla, Bingwa wa upasuaji wa
mifupa, Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani (Physician) n.k.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema
kuwa katika Mkoa wa Pwani Serikali imejenga na kuboresha vituo vya Afya zaidi
ya 16, Hospitali za Wilaya 3, na kuboresha Hospitali ya Mikoa ili kuwa na
huduma za wagonjwa mahututi na wagonjwa wa Dharura.
Mbali na hayo Waziri Ummy amewahasa
Mwananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afyà ili kujihakikishia matibabu wakati
wa ugonjwa, jambo litalosaidia kuokoa gharama kubwa za matibabu pindi Mwananchi
anapopata ugonjwa.
“Nitoe Wito kwa Wananchi kujenga
utaratibu wakujiunga na Bima ya Afya, kwasababu ndio njia ya uhakika
yakujihakikishia matibabu kabla hawajaugua” alisema Waziri Ummy.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akieleza Waandishi wa Habari (hawapo kwenye
picha) umuhimu wa kifaa kinacho rekodi mahudhurio na muda wa watumishi kufika
ofisini (Biometric) wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji
huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari
Bingwa wa Hospitali teule ya Mkoa wa Pwani Tumbi, baada ya kumaliza ziara yake
ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment