NA
HADIJA HASSAN, LINDI
Naibu
waziri wa Nishati Subira Mgalu amezitaka Shule Zote Nchini zinazowekewa miundo
mbinu ya Umeme kupitia mradi wa umeme Vijijini (REA) , kuutumia umeme huo
kuongeza ufaulu katika Shule zao.
Mgalu
ameyasema hayo jana alipokuwa anazungumza na baadhi ya wanafunzi na walimu
katika shule ya Sekondari Mnacho kijiji cha Luchelegwa Wilayani Ruangwa Mkoani
Lindi wakati wa hafla fupi ya kuwasha umeme katika shule hiyo.
Mgalu
amesema ili umeme huo uweze kuleta tija ni wajibu kwa walimu kuongeza kasi ya
kufundisha na wanafunzi kujisomea kwa kutumia muda wa ziada hata nyakati
za jioni
“Serikali
inapoamua kufanya maboresho katika maeneo haya ina nia ya makusudi ya kutaka
kuona mabadiliko maana sasa hamtakuwa na kisingizio tena cha kufanya vibaya ”
alisema Mgalu.
Pamoja
na mambo mengine Mgalu alitumia fursa hiyo kuwaasa wanafunzi wa shule
hiyo kusoma kwa bidii ili kupata matokeo mazuri , pamoja na kuwataka
wanafunzi wa kike kuepuka vishawishi kwa vijana wa kiume
“Nawaomba
msome watoto wangu hasa watoto wa kike, mshika mawili moja humponyoka ni aibu
sana tukionekana mikoa ya kusini na ukanda huu kwamba sisi wanafunzi wetu wengi
wanafeli kwa sababu ya kupata ujauzito wakati tupo sisi wenzenu wa mfano
tumetoka kusini na tulivumilia hizo mimba tulikuja kuzipata baadae baada ya
kuanza maisha yetu” alisema Mgalu
kwa
upande wake mkuu wa Shule hiyo David Mwakalobo alisema kuwa kabla ya kuwekwa
kwa umeme huo shule hiyo ilikuwa inatumia umeme wa jua ambao ulikuwa haukidhi
mahitaji kwani walikuwa walikuwa wanalazimika kutumia kompyuta tano tu kati ya
ishirini walizonazo wakati wa kufundishia kutokana na uwezo mdogo wa
nishati iliyokuwa inatumika
Mwakalobo
Alisema umeme huo Licha ya kuutumia katika masomo hayo ya kompyuta pia
wanatarajia kununua shajala itakayoweza kudurufu Mitihani hali ambayo
itawarahisishia Wanafunzi kutotumia muda mwingi kuandika Mtihani kwenye
Makaratasi pamoja na Walimu kuweka kwa usiri wa mitihani hiyo huku
ikiwarahisishia Walimu kutoandika kwa chaki ubaoni wakati wa Mitihani hiyo.
Aliongeza
kuwa wanaishukuru Serikali kwa kuwawekea umeme katika shule yao kwani utaweza
kuongeza kiwango cha ufaulu kwa kuongeza ubunifu wa ufundishaji kwa walimu
Kufuatia
hatua hiyo ya kuwasha umeme katiaka Shule ya Sekondari Mnacho Mkandarasi
anaetekeleza mradi huo wa kusambaza umeme vijijini (REA) STATE GRID amehaidi
kuweka mfumo wa umeme katika shule hiyo.
No comments:
Post a Comment