Na
Hadija Hassan, Lindi
Halmashauri
ya Wilaya ya Lindi mkoani humo imewashauri Mfuko wa Misitu Tanzania (Tanzania
Forest Fund) kurejesha kwa wakati fedha za upandaji Miti ili kuendelea
kupambana na Mabadiliko ya Tabia Nchi
Wito
huo umetolewa na afisa Aridhi na Maliasili wa Wilaya hiyo Victor
Shau leo alipokuwa anazungumza na Bagamoyo kwanza ofisini kwake
Amesema
ni vema fedha hizo zikalejeshwa kwa wakati ili ziweze kusaidia katika
miradi midogomidogo hasa kwa kuanzisha vitalu vya upandaji wa miti
Alisema
fedha hizo kwa kiasi kikubwa zinatokana na makusanyo yao kama Halmashauri
katika mavuno ya Mazao ya misitu
Kwa
upande wake Afisa Maliasili wa Wilaya hiyo Chares Mwaipopo alisema
kuwa katika kipindi cha mwezi may 2017 hadi mwezi june 2018 Halmashauri hiyo
iliweza kukusanya kiasi cha milioni 29.178191 ambapo walitakiwa kurejeshewa
kiasi cha shilingi milioni 78468.50
Hata
hivyo BAGAMOYO KWANZA BLOG ilipomtafuta afisa Misitu wa wakala wa misitu TFS
Wilaya ya Lindi, Oswald Laswai
alikili wilaya hiyo kucheleweshewa mrejesho wa Fedha zao za mavuno ya
mazao ya misitu ambapo amesema kuwa ucheleweshwaji wa fedha hizo kwa
kiasi kikubwa unatokana na wahusika kuchelewa kupeleka madai katika mfuko huo
No comments:
Post a Comment