Tuesday, February 19, 2019

CCM YABOMOA NGOME YA CUF RUFIJI.

Na Shushu  Joel,Ikwiriri.
..................................
CHAMA cha mapinduzi (Ccm) wilaya ya  Rufiji  mkoani Pwani kimefanikiwa kuibomoa ngome  ya upinzani katika wilaya hiyo  ilikuwa imeota mizizi.

Akizungumza na viongozi wa  matawi wote wa wilaya hiyo katibu wa chama  hicho Mtua alisema kuwa chama cha cuf  kilikuwa na ngome kubwa  katika wilaya hii  lakini tangu  wannachi  hao waone  utekelezaji wa Ilani ya Ccm chini  ya  mwenyekiti  wa Taifa ambaye pia ni Rais  wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ambaye amekuwa mstali wa mbele katika uletaji wa maendeleo kwa wananchi.

Alisema kuwa awali watu  walishindwa kujiunga na Ccm kutokana na ahadi nyingi kutokamilika kwa wakati lakini kipindi hiki  yote yamefanywa na yanaendelea kufanyika.

"Rufiji ilikuwa ni ngome kuu ya chama cha upinzani cha Cuf lakini kwa  muda  wa miezi michache nilianza kazi hapa kama Katibu nimefanikiwa kuvuna wanachama zaidi ya 1000 hivyo inaonyesha ni jinsi gani ngome hiyo inavyoputikika" Alisema Mtua.

Aidha  aliongeza  kuwa bado  kunanafasi za kutosha kwa wale wanaohitaji kujiunga na Ccm kwani ni chama pekee chenye kuwajali  wananchi pasipo  ubaguzi wa kabila kama ilivyo kwa vyama vingine.

Kwa upande  wake diwani wa kata ya Ikwiriri Ally Ndungutu ambaye awali alikuwa ni diwani kupitia Cuf lakini amejiunga Ccm alisema kuwa kuna kundi zaidi ya elfu 10 wanakuja kujiunga na Ccm sema  tu wanasita sita  lakini watakuja.

Aliongeza kuwa alipokuwa  Cuf kuna  vitu vingi  alikuwa havipati kutokana chama hicho kutokuwa  na vikao vya ushauri na mwelekeo wa maendeleo kwa Taifa.

Hivyo amewataka watanzania  wote nchini kujitathimini kwa yale wanayotendewa  na Rais wa awamu ya tano.

Naye Mwanahasi Geruka mkazi wa Ikwiriri amempongeza katibu wa ccm wilaya hiyo  kwa juhudi zake anazozifanya za uvunjaji wa ngome  ya upinzani  katika wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment