Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwaonyesha jengo la TAMISEMI (halipo pichani)
wakati wa ziara yake na Makatibu Tawala, Wenyeviti wa halmashauri na
Wakurugenzi kuwaonyesha mfano bora wa matumizi ya Force Account.
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Rais TAMISEMI
linaloendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa.
............................................
Majid Abdulkarim
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameonyesha matumizi bora ya utekelezaji wa miradi bila kutumia mkandarasi maarufu kama ‘Force Account ‘ kwa Makatibu Tawala wa Mikoa ,Wenye viti wa Halmashauri, Wakurungezi na Maafisa mipango wa Halmashauri kwa kuwapeleka kwenye mradi wa Ofisi za Jengo la Ofisi ya Rais TAMISEMI linaloendelea kujengwa katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
Jafo amefanya ziara hiyo baada ya kikao chake cha maelekezo kwa viongozi hao ambao halmashauri zao zilifaulu vigezo na kusaini fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati awamu ya Pili.
Akizungumzia Force Account Jafo alisema kuwa nimeamua kutekeleza kwa vitendo yale ninayowaagizaga wakati wote wa maelekezo yangu kuhusu kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yenu.
Katika ujenzi wa Jengo hili la Ofisi za Wizara tuliamua na kukubaliana kwa pamoja kutumia mfumo ule ule ambao unatumika katika halmashauri zetu sio sisi tunatoa tu maagizo lakin hatutendi na sasa kupitia mradi huu tumeamua kuwa mfano halisi wa yale tunayoyazungumza alisema Jafo.
Aliongeza kuwa katika mfumo huu wa force Account tumeweza kusimamia jengo hili kupitia kamati nne ambazo ni Kamati ya manunuzi, Kamati ya Vifaa, Kamati ya ujenzi na ile ya usimamizi na ufuatiliaji.
“Mradi huu umekuwa na tija pia kwa jamii kwani umetengeneza ajira kwa vijana wetu kwani wao ndo wamekua nguvu katika kufanya shughuli zote za ujenzi kuendelea kwa mujibu wa maelekzo ya wahandishi ambao wanatokea Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na msimamizi wa mradi huu”Amesema Jafo.
Wakati huo huo Jafo aliongeza kuwa ujenzi wa Jengo hili la kisasa zaidi linagharimu shilingi billion moja tu Fedha zilizo tolewa na Rais Magufuli kwa kila Wizara kwa ajili ya kujenga Ofisi katika Mji wa Serikali Ihumwa.
“Nataka niwahakikishie kuwa ujenzi wa
jengo hilo umeratibiwa na mimi mwenyewe Waziri wa TAMISEMI ambapo
niliwaunganisha viongozi wote wakuu wa Wizara pamoja na watendaji wa Wizara ili
kuleta matokeo makubwa na ya haraka”
Sasa kama mimi
nimeweza wewe kwanini ushindwe na jengo hili limeanza kujengwa mwezi Disemba
2018 na kama mnavyoona sasa hivi jengo limeshafikia hatua ya mtamba wa panya
kwahiyo kasi ya ujenzi iko vizuri sana na tutamaliza ujenzi huu ndani ya muda
mfupi ujao; Nataka na nyie mkafanye hivi kwenye maeneo yenu alimalizia Jafo.
Kwa kuongezea
Jafo amazitaka halmashauri zilizo pata fedha ya kutekeleza miradi ya Kimkakati
kuanza mipango ya utekelezaji wa miradi hiyo mapema iwezekanavyo ili fedha hizo
zitakapo wasili katika halmashauri hizo miradi ianze mara moja na ili iweze
kumalizika kwa wakati ulopangwa.
Aidha naye
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Eng.. Zenah Saidi ametoa shukrani za dhati kwa
Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa fedha
hizo na kuhaidi kusimamia kwa umakini na kuhakikisha zinatekeleza miradi huska
kwa ufasa na ubora wa miradi hiyo kuendana na thamani ya fedha hiyo.
“Ni toe wito kwa
viongozi wa halmashauri kuwa sasa ni wakati wa kutekeleza miradi hii kwa
kutumia mfumo wa Force Account kwani kila mmoja wetu kapata kushuhudia kwa
macho yake namna ya mfumo huu unavyo tumika na faida zake kazieleza Bi.Zenah.
Kwa kuhitimisha
Bi.Zena amewataka viongozi wenzake kuwa makini wakati wa kutafuta wakandarasi
wa kutekeleza miradi kwa wengi wao katika makaratasi wanakuwa vizuri lakini
katika utekelezaji hakuna kitu.
No comments:
Post a Comment