Chama cha Mapinduzi Wilaya ya
Bagamoyo kimeadhimisha miaka 42 ya siku ya kuzaliwa kwa chama hicho kiwilaya
katika kata ya Pera kijiji cha Pingo katika Halmashauri ya wilaya ya Chalinze
kwa kufanya usafi katika eneo la Ujenzi wa shule ya sekondari ya Pera
inayojengwa kwa nguvu za wananchi na kituo cha afya cha Pingo.
Maadhimisho hayo yamepambwa na
wananchi,vikundi mbalimbali vya sanaa na wanachama wa chama cha Mapinduzi kutoka Halmashauri Zote mbili wilayani Bagamoyo na
Vijana wa chama cha Mapinduzi ambao waliandamana kutoka eneo la Ujenzi wa shule
ya sekondari ya Pera hadi eneo la mkutano katika viwanja vya kijiji cha Pingo.
Maandamano
hayo yaliyoongozwa na Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Bagamoyo
Bwana John Francis Masenga na kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Bagamoyo Bwana Sheriff Zahoro.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo
katika hotuba yake aliyasema mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha
Mapinduzi kitaifa lakini pia katika ngazi ya wilaya kwa kuyasema mafanikio
yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Chama cha Mapinduzi katika
nyanja mbalimbali za maisha hususan katika sekta za Elimu, Afya na utoaji
huduma kwa wananchi Kwani watumishi wa serikali wamekuwa waadilifu na wanatoa
huduma kwa wananchi kwa wakati.
Aidha aliwashukuru madiwani, wabunge
na Mkuu wa wilaya kwa usimamizi na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi
na Mwisho aliwataka wananchi kuendelea kuiunga Mkono serikali ya awamu ya tano
chini ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Bagamoyo Bwana Sheriff Zahoro akizungumza katika maadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment