Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)
akisisitiza uadilifu kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, wakati
wa kikao kazi na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
............................
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amemuonya Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mkuranga, Bw. Valintine Mbai ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na
Rasilimali watu wa Halmashauri hiyo kuacha tabia mbaya ya kutumia cheo
chake kuomba rushwa ya ngono kwa Watendaji wa Vijiji katika Halmashauri hiyo na
kumtaka afisa huyo kubadili mwenendo wake haraka iwezekanavyo.
Onyo hilo
amelitoa wilayani Mkuranga, wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mkuranga chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla ya kuanza
kutembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika halmashauri hiyo
ili kujiridhisha na utekelezaji wake.
Akizungumza
na watumishi hao, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, ni aibu kwa afisa huyo mwenye
dhamana ya kusimamia maadili ya kiutumishi kutumia madaraka yake vibaya kwa
kuomba rushwa ya ngono toka kwa Watendaji wa Vijiji jambo ambalo ni kinyume cha
maadili ya kiutendaji katika utumishi wa umma.
Amemtaka
afisa huyo kuacha tabia hiyo na kujirekebisha maramoja ili awe mfano bora kwa
watumishi anaowasimamia kimaadili.
Pi
amemtaka, afisa huyo kuwa na heshima kwa wakuu wake wa kazi akiwemo Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo ili kutengeneza mazingira mazuri ya kiutendaji.
Aidha, Mhe.
Dkt. Mwanjelwa ametoa angalizo kwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Juma
Abeid kutowatetea watumishi wasio waadilifu na badala yake awachukulie hatua za
kinidhamu hata kama ni marafiki zake.
Mhe. Dkt.
Mary Mwanjelwa (Mb) ameendelea kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma
nchini akiwa wilayani Mkuranga na kutoa wito kwa watumishi wote wa umma
kuhakikisha wazingatia Kanuni za Maadili ya Utendaji Kazi katika Utumishi wa
Umma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza
hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mkuranga, wakati wa kikao kazi na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji
No comments:
Post a Comment