Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo yapitisha Makadirio ya beti ya
2019/2020 Kutumia Kiasi cha Tsh Billioni 84.6 kwa mwaka wa fedha
2019/2020.
Akisoma Hotuba yake Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo,Mh Boniface Jacob,
amefanunua kuwa katika pesa hizo serikali itatoa ruzuku ya Billioni
65.5,Millioni 750 ni michango ya Wananchi na billioni 18.4 ni Makusanyo
ya ndani.
Ambapo katika matumizi yake fedha hizo,Billioni 72.3 ni Mishahara ya
watumishi,Na kiasi cha billioni 12.3 zimeelekezwa katika miradi
Mbalimbali ya Maendeleo
Aidha ameweka msisitizo kuwa Kiasi cha billioni 8.3 sawa na Asilimia
60,za mapato yanayokusanywa na Halmashauri zitatumika kwa ajili ya
Miradi ya maendeleo
Mstahiki meya ametaja Vipaumbele 11 vya Halmashauri vilivyomo katika Bajeti hiyo
kuboresha utoaji huduma kwa jamii kwa kuongeza pesa za kujengea Makao
makuu ya Halmashauri kiasi cha Millioni 700, Kuanza kujenga Hospitali ya
wilaya kwa kiasi cha Tsh Millioni 250
Kutenga fedha za kujenga machinjio ya kisasa kiasi cha Tsh Millioni 250
pia Kutenga fedha Kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Mbezi ( kwa ajili ya
wamachinga) Kiasi cha Tsh millioni 300.
Kuimarisha Utawala bora kwa kuwatengea fedha za kiinua Mgongo wenyeviti wa Serikali za mitaa wanaomaliza muda wao mwaka 2019
Kuongeza Mapato kwa kuboresha miundombinu ya ukusanyaji, kubuni vyanzo
vipya, Uanzishaji wa stendi za daladala Mloganzila na Msumi, Uanzishwaji
wa Masoko mapya Kiasi cha Tsh Billioni 1.7 zimetengwa
Kuongeza kiwango cha Uzoaji taka Ngumu kwa manispaa kwa Kununua Vifaa
vya ubebaji taka kama magari na mitambo,Kiasi cha Tsh billioni 3.02
kimetengwa
Ujenzi wa Mabweni ya Wavulana na Wasichana shule ya Sekondari Goba TshMillioni 230 zimetengwa
Kutoa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake,Vijana na Walemavu Kiasi cha Tsh billioni 1.38 zimetengwa
Kupima maeneo ya Umma,kwa kutoa hati miliki na kutwaa Maeneo ya miradi ya uwekezaji Kiasi cha Tsh billioni 1.4 zimetengwa
Kwa kuboresha na Kujenga Miundombinu ya Elimu Msingi na Sekondari kwa
kujenga madarasa na Nyumba za walimu,Kiasi cha Tsh billioni 1.168
zimetengwa kwa kazi hiyo.
Aidha Mstahiki meya amesisitiza kuwa,Halmashauri ni chombo cha wananchi
ambacho kimewekwa kisheria katika kukuza uchumi na kusogeza ajira kwa
Vijana ili kupunguza Umasikini hasa wa kipato ili Kujiletea Maisha Bora
IMETOLEWA Na
OFISI YA MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA UBUNGO
No comments:
Post a Comment