Tuesday, February 5, 2019

CHANEL TEN NI MALI YA CCM SASA - JPM

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi  (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafanyakazi na Watangazaji wa Channel Ten na Radio Magic Fm,  alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM kwa sasa, Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5, 2019.
 

.................................................



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. John Magufuli ameahidi kutoa milioni 200 kwaajili ya kuboresha Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten kilichpo chini ya African Media Group (AMG) ambacho kwa sasa ni mali ya CCM.


Katika kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa alifuatana na mkewe mama Janeth kutembelea kituo cha Televisheni cha Channel Ten


“Nimeona leo katika kuadhimisha miaka 42 ya chama nipite hapa kuwasikiliza na kufahamiana nanyi japo wengine nawaona tu kwenye TV, kwakweli mnafanya kazi nzuri pamoja na changamoto zilizopo hongereni sana” alisema Rais Magufuli.


Dkt. Magufuli amesema anatambua juhudi kubwa zinazofanywa na wafanyakazi wote wa Channel ten, Magic FM, pamoja na vyombo vya habari vyote vilivyoko chini ya African Media Group na ameahidi kuwasaidia kwa hali na mali ili kutekeleza majukumu yao kwa maslahi ya nchi. 


Aidha Rais Magufuli ameahidi kuwanunulia vifaa vipya pamoja na kuwatafutia jengo jipya litakalotumika kurushia matangazo ili kuwezesha vyombo hivyo vya habari kusikika nchini kote na kimataifa.


“Nimeamua kuwapatia shilingi milioni mia moja kwaaajili ya kununulia vifaa, pia nitawaongezea nyingine mia ili ziwe miambili hii yote ni kwaajili ya kuimarisha utendaji wenu” Alisema Rais Magufuli. 
 

Dkt. Magufuli aliwaasa uongozi wa vyombo hivyo vya habari vya chama cha mapinduzi kutojaribu kufanya ubadhirifu katika fedha alizotoa kwani watakuwa wamekosa uzalendo lakini pia watajulikana na watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kampuni ya African Maedia group (AMG) ambao ni wamiliki wa kituo cha televisheni cha Chane ten, DTV, Magic FM vyote vya jijini Dar es Salaama sasa vinamilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).


kufuatia hatua hiyo, CCM sasa wanamiliki vyombo vya Habari  vifuatavyo vya habari.
1.Gazeti la Uhuru
2.Gazeti la Mzalendo
3.Radio Uhuru
4.Channel Ten
5.Magic FM
6.CTN
7.DTV.


Rais aliwataka wafanyakazi wa kampuni hiyo kuchapa kazi kwa bidii ili kuzalisha faida na hatimaye kujiendesha kwa tija kwa manufaa ya watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama wala imani.
 
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufguli na Mkurugenzi mtendaji African Media Group (AMG) Jaffari Haniu wakimsikiliza mtangazaji wa kituo cha Channel Ten Hanifa Roy alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth wakimsikiliza mtayarishaji vipindi wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten Issa Didi alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji African Media Group (AMG) Jaffari Haniu alipotembelea ili kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5,2019.
Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumzana Wafanyakazi na Watangazaji wa Channel Ten na Radio Magic Fm,  alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam.Febuari 5, 2019.

Mama Janeth Magufuli Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimu Wananchi mbalimbali waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm,  walipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group
Wananchi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliwapokuwa akizungumza nao Wananchi hao waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm,  alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam. Febuari 5, 2019.
Wananchi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliwapokuwa akizungumza nao Wananchi hao waliokuwa nje ya Ofisi za Channel Ten na Radio Magic Fm,  alipotembelea kuangalia utendaji kazi wa Vituo vya Televisheni na Radio vya African Media Group vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi CCM. Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 42 ya CCM. Jijini Dar es Salaam. Febuari 5, 2019.

No comments:

Post a Comment