Kutoka
Kushoto alievalia suti ya Blue ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga
katika ni Mzee Athumani Nadonde mnufaika wa kaya masikini kijiji
cha Maumbika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi akitoa maelezo
mafupi kwa Waziri wa Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora George Mkuchika ya namna alivyofanikiwa kuweka Bati katika Nyumba yake
......................................
NA HADIJA HASSAN, LINDI.
Serikali imesema kupitia Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii TASAF awamu ya iii B imedhamiria kuwafikia walengwa wote wanaostahili
kuingizwa kwenye Mpango wa kunusuru kaya masikini
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawara bora kapteni msaafu George Mkuchika jana
alipokuwa akizungumza na wakazi wa kata ya Mahumbika Halmashauri ya Wilaya ya
Lindi Mkoani Humo.
Mkuchika alisema awamu hiyo ya tatu B inatarajiwa kuanza
mapema katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 na kwamba Serikali imekwishafanya
maandalizi ya jambo hilo.
Alisongeza kuwa changamoto kubwa iliyokuwepo kwa TASAF
ni Kutowafikia walengwa wote katika Vijiji ambapo mpaka sasa ni asilimia 70 tu
ndiyo waliofikiwa huku 30% wakiwa bado kufikiwa.
Ameongeza kuwa katika mpango huo wa kunusuru kaya masikini
licha ya Baadhi ya Wananchi kutonufaika na mradi katika maeneo yao pia vipo
vijiji vingine ambavyo havijafikiwa kabisa na Mpango huo huku akiwataka
wananchi ambao wako kwenye mpango lakini bado hwajafikiwa kuwa wavumilivu.
Awali akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa mpango wa kunusuru
kaya masikini (TASAF 3) Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga alisema
Halmashauri ya wilaya ya Lindi ni miongoni mwa Halmashauri zinazotekeleza
Mpango wa Kaya Masikini ambapo jumla ya kaya 9732 ziliandikishwa katika vijiji
88 viliivyoingizwa kwenye mpango kati ya vijiji 140 vilivyopo
katika Wilaya hiyo.
Hata hivyo Ndemanga alisema kuwa idadi hiyo imeendelea
kupungua kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo , vifo, kuhama pamoja na
uhakiki endelevu ambao umekuwa ukiwaondoa walengwa waio na sifa za kuendelea
kuwemo kwenye Mpango
Aidha amesema hadi kufikia Novemba-Disemba 2018 idadi za
kaya zinazoendelea kunufaika na mpango huo wa kunusuru kaya masikini ni 8,842
katika vijiji 88 vya Wilaya hiyo.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Lindi amebainisha pia kuwa
katika mpango huo baadhi ya Walengwa wameweza kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha
shughuli ndogo ndogo za uzalishaji mali na kuboresha makazi yao lakini pia
wamejiunga katika vikundi vya kuweka na kukopa.
Akitoa ushuhuda mbele ya Waziri Mkuchika Athumani
Nandonde mnufaika wa Mpango huo wa kumusuru kaya masikini aliishukuru Serikali
kwa kuanzisha mpango huo kwani kupitia fedha anazozipata kutoka TASAF ameweza
kuweka bati katika nyumba yake huku akiwahasa walengwa wezie kutumia fedha
wanazozipato kupitia mpango huo kuzitumia katika mambo ya maendeleo
Muonekano
wa Nyumba ya Mzee Athumani Nandonde Mnufaika wa Mpango wa kunusuru kaya
masikinj Mkazi wa kata ya Maumbika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani
Lindi
No comments:
Post a Comment