MJUMBE wa mkutano mkuu wa chama cha
mapinduzi (CCM) kupitia mkoa wa Pwani Haji Jumaa alisema kuwa kipindi
hiki cha uchaguzi awana wasiwasi wa aina yeyote yule kuhusu
viongozi wao kuchaguliwa.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati wa mkutano wa
viongozi wote wa chama hicho katika kata ya Nianjema wilaya ya Bagamoyo mkoani
Pwani ambapo walikuwa wakijadili kile walichowafanyia wananchi
tangu kuchaguliwa kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Aliongeza kuwa usemi huo unatokana na kile
kilichoahidiwa kwa wananchi na viongozi wetu kipindi walipokuwa
wakiomba ridhaa ya kuongozi na jinsi walivyotekeleza ahadi zao.
"Naamini chaguzi zijazo CCM itashinda kila
kitongoji bila kupoteza hata kimoja kutokana na uwepo wa utitili wa
maendeleo kwa wananchi kuwa ya uhakika na huduma walizokuwa wakizihitaji
kuwafikia"Alisema Jumaa.
Aliongeza kuwa kutokana na kazi kubwa
inayofanywa na mwenyekiti wa Ccm taifa ambaye pia ni Rais wa Tanzania Dkt
John Pombe Magufuli kuwa mstali wa mbele katika utekelezaji wa miradi ya
maendeleo kwa wananchi kazi ya uchaguzi ujao itakuwa kama tunasukuma
mlevi.
Aidha aliongeza kuwa kwa mkoa wote Ccm
imejipanga kuwa na viongozi imara na watakao kuwa ni chaguo sahihi la
wananchi na watakao waletea maendeleo wanayoyahitaji.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo ya Nia njema Abdul
Pyalla amempongeza Mnec huyo kwa jinsi alivyoelezea mambo mengi
yaliyofanywa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kipindi
hiki na hivyo kuwarahisishia wagombea .
Aliongeza kuwa kwa kata ya Nia njema kuna mengi yamefanyika
ikiwemo kujenga shule moja ya msingi, kituo cha Afya na shule ya
sekondari pia wamefanikiwa kuchimba visima tisa vya maji na
ukarabati wa barabara za mitaa.
Akitoa maelezo shukurani kwa viongozi na wanachama wa
chama hicho katibu wa Ccm wilaya hiyo Salum Mtelela alisema kuwa pindi
watakapo pata waraka wa uchaguzi wanachama wote
watapewa taarifa kwa lengo la kuwapata viongozi ambao ni
chaguo sahihi la wananchi.
No comments:
Post a Comment