Mbunge
wa Viti Maalumu kupitia chama cha mapinduzi CCM Manispaa ya Lindi,
Hamida Abdala, ametoa msaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika
shule ya msingi Mpilipili iliyopo Lindi Mjini.
Ametoa
msaada wa viroba 3 vya unga, kiroba 1cha Sabuni, Maharage, Maziwa na
Madaftari kwa wanafunzi wenye uhitaji maalumu ikiwa ni njia mojawapo ya
kuwapa moyo wa kujiona wapo sawa na wanafunzi wengine na kuwapa moyo wa
kupenda shule bila kujali mazingira wanayoishi.
Aidha
Mbunge huyo amesikitishwa na uchakavu wa jengo linalotumiwa na
wanafunzi hao na kusema atakutana na Mkurugenzi wa Manispaa waweze
kuweka mazingira mazuri na kuahidi kuongeza madawati wanafunzi hao.
“Nasikitika
kuona uchakavu wa darasa licha ya kuwa ni moja ambalo tumeshindwa
kulisimamia na naahidi nitakutana na Mkurugenzi wa Manispaa ili tuweke
katika hali nzuri na yenye usalama kwa maendeleo yenu kitaaluma,”
amesema Mbunge huyo .
Ametaja
changamoto nyingine ya upungufu wa madawati na ameahidi kuitatua na
amewaomba viongozi wengine wawe na hali ya kutembelea mashule mbalimbali
ili waweze kugundua changamoto zinazowakabili wanafunzi ili zitatuliwe
na wanafunzi wapate matokeo mazuri kwenye mitihani yao.
Kwa
upande wake mwl. Fadhili Saidi Mtitima ametoa pongezi kwa Mbunge wa
viti maalumu kwa kuwapatia zawadi licha ya kusahaulika kwa kundi hilo
lenye uhitaji maalumu na ametaja idadi ya wanafunzi hao jumla ni 32 huku
wasichana wakiwa 10, wavulana 22 na hali ya kitaaluma wapo vizuri hivyo
ameomba wazazi wawapeleke watoto wao wasiwafiche majumbani waende
wakapate elimu yao ya msingi

No comments:
Post a Comment