Na
Omary Mngindo, Chalinze
SERIKALI
imesema kuwa, hatua ya kudhibiti upakizi wa lasirimali za misitu kutoka ujazo
wa kilo 110 mpaka 50, inalenga kulinda wakulima, ambao walikuwa wanapunjwa na
wafanyabiashara.
Hayo
yameelezwa na Sadala Ally Afisa Misitu (DFO) Idara ya Ardhi na Maliasili
Halmashauri ya Chalinze Bagamoyo Pwani, akitolea ufafanuzi wa swali la Madiwani
waliotaka kufahamu sababu za kupunguzwa ushuru kutoka shilingi 24,000 mpaka
kiwango kinachotozwa hivi sasa.
"Kabla
ya mabadiliko ya sheria ile, kulikuwa na utozwaji wa kati ya sh. 24,000
ikaja 16,000 baada ya mabadiliko ikaja sh. 12,000, hatua hii inalenga
kuwanusuru wakulima waliokuwa wanadhulumiwa na wafanyabiashara," alisema
Sadala.
Ameongeza
kuwa kupitia mabadiliko ya pesa ya mwaka jana, serikalu ikatoa maelekezo
kupitia gn namba 46 ikatoa maelekezo kwamba halmashauri zitoze asilimia 5
kinachouzwa kutoka kunakozalishwa.
Katika
Baraza hilo Madiwani walielekeza malalamiko katika idara ya Ardhi ambayo
imedaiwa kushindwa kumaliza migogoro kati ya vijiji na vijiji hali na mingine
inayowahusu wananchi wa kawaida, ambapo baadhi yao inahatarisha usalama katika
halmashauri hiyo.
Madiwani
Malota Kwaga, Rehema Mwene na Lucas Lufunga kila mmoja alielezea masikitiko
yake kuhusiana na migogoro ya ardhi, huku Lufunga akilalamikia hati za viwanja
vilivyopimwa katika eneo la Kibiki Kata ya Bwilingu Mamlaka ya Mji Mdogo wa
Chalinze.
Mkuu
wa wilaya hiyo Zaynabu Kawawa alitoa siku tatu kwa maofisa wa ardhi kuwasilisha
vielelezo kwa maandishi kuelezea namna walivyoshughulikia migogoro hiyo.
Afisa
Ardhi Mteule Zefania Sabo aliliambia baraza hilo kwwamba aliliwasilisha suala
la viwanja katika eneo la Kibiki katika Kamati ya fedha, huku akitaka
iwasilishwe kwenye baraza lijalo.
No comments:
Post a Comment