Monday, February 4, 2019

MADIWANI LINDI WATAKIWA KUSHIRIKIANA

Na Hadija Hassan, Lindi.

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani Humo wametakiwa kuacha itikadi za vyama vyao na Badala yake  wadumisha Mshikamano kwa maslahi ya Manispaa yao

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Lindi Saidi Madebe  alipokuwa akitoa salamu za Chama hicho juzi katika kikao cha Robo ya pili cha Baraza la Madiwani

Madebe alisema ili Manispaa hiyo iweze kuwa na maendeleo ni vyema Madiwani wakawa wanaushirikiano wenyewe kwa wenyewe pamoja na watumishi wengine

“sisi ndio tuliopewa dhamana na wananchi hivyo ni vizuri tukiwa tunashirikiana pamoja na kushirikishana katika shughuli za kuwaletea Maendeleo Wananchi wetu  ikiwapamoja na kubuni kwa pamoja mbinu mbali mbali za kuongeza kipato ndani ya Halmashauri yetu” alisema Madebe

Madebe aliongeza kwa kuzingatia kuwa Manispaa yao kuwa masikini wa vyanzo vya Mapato ni vyema madiwani na watumishi kubuni mbinu mbali mbali za kuanzisha miradi ya uvunaji wa mazao ya bahari au mashamba

 “kutokana na uhalisia wa Halmashauri yetu njia kubwa ya kuongeza kipato ni hiyo kupitia Bahari na Mashamba hivyo ni vyema ni  kubuni miradi au kutafuta wawekezaji ili kuwekeza katika eneo hilo kwa hakika mkishirikiana kwa pamoja kwa wazo hili au linguine tunaweza kuongeza kuongeza vyanzo vya mapato pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi wetu” Alisisitiza  Madebe


No comments:

Post a Comment