Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa, akishiriki ujenzi wa vymba vya madarasa shule ya sekondari Pera Halmashauri ya Chalinze, aliyesimama kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Saidi Zikatimu.
............................
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawaamewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka shule watoto wote
waliofaulu kuingia kidato cha kwanza ifikapo jumatatu ya tarehe 04 Mach 2019.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa tamko hilo wakati
akizungumza na viongozi wa kata na tarafa katika Halmashauri ya Chalinze na
kuwataka viongozi hao wasimamie maagizo hayo.
Tamko hilo limekuja baada ya shughuli za ujenzi
wa vyumba vya madarasa zikiendelea wilaya yote ya Bagamoyo lengo likiwa ni
kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakaekosa masomo kwasababu ya upungufu wa vyumba
vya madarasa.
Katika ziara yake hiyo ya kukagua ujenzi wa
vyumba vya madarasa, Mkuu huyo wa wilaya ameshiriki shughuli za ujenzi katika
shule ya Sekondari Pera kata ya Pera Halmashauri ya Chalinze ambapo ujenzi wake
unaendelea.
Wakati hyuo huo Mkuu huyo wa wilaya Zainabu
Kawawa amesema kila mzazi anapaswa kusaini mkataba maalum wa kuthibitisha kuwa
mtoto wake atasoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne bila ya kukosa.
Katika zoezi hilo la kusaini mikataba amewaagiza
maafisa tarafa kusimamia na mzazi au mlezi atakaekwenda kinyume atachukuliwa
hatua za kisheria.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa kata na tarafa na wanachi wanaoshiriki ujenzi wa shule ya sekondari Pera Halmashauri ya Chalinze, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Saidi Zikatimu.
No comments:
Post a Comment