Na
Hadija Hassan, Lindi.
Mahakama
ya wilaya ya Lindi, Mkoani Lindi, imemuhukumu mkazi wa Kijiji cha Milola,‘B’
Salum Kunyuma (26) kifungo cha miaka (20) Gerezani,baada ya kupatikana na hatia
ya kumdhalilisha kimapenzi Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu Jina
limehifadhiwa.
Hukumu
hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Franco Kiswaga, kufuatia mshitakiwa
kukiri kosa aliloshitakiwa nalo bila ya kulazimishwa.
Kabla
ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Hakimu Kiswaga alimpa mshitakiwa nafasi ya
kujitetea ambapo aliiomba Mahakama hiyo isimpe adhabu kali kwa maelezo
alilazimika kutenda kosa hilo,baada ya kukaa muda mrefu bila ya kukutana
kimapenzi na mwanamke yeyote.
Baada
ya utetezi huo,Kiswaga alimuuliza Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Godfrey
Michael Mramba, kama ana kumbukumbu ya makosa ya zamani kwa Mshitakiwa na
kujibu hana, lakini aliiomba mahakama kumpa adhabu kali, kwani kitendo
alichokifanya ni cha kinyama dhidi ya Mtoto mdogo asiye na hatia.
Hakimu
Kiswaga akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 12/2019, kupitia vifungu vya
Sheria 138 (C) kifungu cha (1) na (2) (b) kanuni ya adhabu sura ya 16,alisema
hakubaliani na utetezi huo kwani wapo wanawake walio sawa na lika lake, hivyo
akamuhukumu kifungo cha miaka (20) Gerezani.
“Sikubaliani
na huo utetezi kwani wanawake walio na umri wako na zaidi yao wapo wengi,hivyo
Mahakama inakuhukumu kwenda Jela miaka (20)”.
Awali
ilidaiwa Mahakamani hapo na Mwanasheria wa Serikali, Mramba aliiambia Mahakama
hiyo kwamba Januari 28 mwaka huu,Mshitakiwa akijua anachokifanya ni
kosa,alikutwa amempaka Mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu,kasha kuchukuwa
uume wake na kuuchuwa Mapajani mwa Mtoto huyo.
Aidha,Mwanasheria
huyo alieleza kuwa Mshitakiwa alipata mwanya wa kufanya kosa hilo kufuatia mama
wa Mtoto huyo,jina limehifadhiwa kumuomba kijana huyo kumuangalizia mtoto
wake wake ,wakati yeye akiwa ameenda Bombani kuteka Maji kwa ajili ya Matumizi
ya Nyumbani.
Mwanasheria
huyo aliiambia Mahakama hiyo kwamba mshitakiwa baada ya kukutwa amempakata huku
akiendelea kujichua juu ya mapaja ya Mtoto wake aliomba msaada wa majirani,na
walipofika walimkuta Mtoto yule akiwa na mbegu za kiume zilizotokana na mwili
wa Kunyumu.
No comments:
Post a Comment