Tuesday, February 5, 2019

CGP. PHAUSTINE KASIKE ATEMBELEA GEREZA KUU LA WANAWAKE TANZANIA – KINGOLWIRA, MOROGORO

 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, (CGP) Phaustine Kasike (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania – Kingolwira, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Loyce Ruhembe  alipotembelea Gereza hilo jana februari 4, 2019 katika ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro.

 Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, Kingolwira, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Loyce Ruhembe akitoa taarifa fupi ya uendeshaji wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania – Kingolwira kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, (CGP) Phaustine Kasike (kushoto meza kuu) jana februari 4, 2019 alipotembelea Gereza hilo.

 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, (CGP) Phaustine Kasike (katikati) akikagua maeneo mbalimbali ya Gereza Kuu la Wananwake (kulia) ni Mkuu wa Gereza Kuu la Wanawake Tanzania, Kingolwira, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Loyce Ruhembe. Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Udereva cha Magereza – Kingolwira, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP). Lazaro Nyanga.
 Askari wa Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira wakiwa timamu kazini wakati Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (hayupo pichani) akizungumza na Wafungwa wa Gereza hilo jana februari 4, 2019 alipotembelea Gereza hilo.

 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, (CGP) Phaustine Kasike (kulia) akiangalia mradi wa kuku wa mayai katika Gereza Kuu la Wanawake Tanzania – Kingolwira alipotembelea jana februari 4, 2019.

 Ujenzi wa nyumba kwa njia ya ubunifu katika Kambi mojawapo ya Gereza Mtego wa Simba, Morogoro ukiendelea katika hatua za awali za ujenzi.

 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, (CGP) Phaustine Kasike akiangalia mashine kufunga majani ya malisho ya mifugo katika mradi wa ng’ombe wa maziwa Gereza Mtego wa Simba.

 Mkuu wa Chuo cha Udereva cha Magereza – Kingolwira, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Lazaro Nyanga akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike (kushoto) majenego mbalimbali yanayokarabatiwa katika chuo hicho kwa kutumia ubunifu
(Picha na Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment