NA
HADIJA HASSA, LINDI
Naibu
Waziri wa Nishati Subira Mgalu amezindua Umeme katika kijiji cha
Namatula kilichopo wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi
kinachopelekewa umeme na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kwa kuwasha katika
shule ya sekondari Namatula
Kuwashwa
kwa umeme katika shule hiyo uwenda utakuwa mwarobaini wa shule hiyo kufanya
vizuri katika mitihani yao ya kitaifa kwa mwaka 2019
Ikumbukwe
kuwa shule ya sekondari ya Namatula ilishika nafasi ya mwisho kitaifa katika
matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 .
Awali
akizungumza na walimu pamoja na wanafunzi Mgalu Alisema uwepo wa umeme huo uwe
chachu ya kufanya vizuri katika mitihani yao ,pamoja na kuhaidi kufuatilia
hatua kwa hatua katika matokeo ya mitihani ya majiaribio,moko na hata ile ya
kitaifa
Mgalu
pia aliwataka wanafunzi wa Shule hiyo kusoma kwa bidii ili kubadilisha
matokeo mabaya ya mwaka uliopita , pamoja na kuwataka wanafunzi wa kike kuepuka
vishawishi kwa vijana wa kiume
“Nawaomba
musome watoto wangu hasa watoto wa kike, mshika mawili moja umponyoka ni aibu
sana tukionekana mikoa ya kusini na ukanda huu kwamba sisi wanafunzi wetu wengi
wanafeli kwa sababu ya kupata ujauzito wakati tupo sisi wenzenu wa mfano
tumetoka kusini na tulivumilia hizo mimba tulikuja kuzipata baadae baada ya
kuanza maisha yetu” alisema Mgalu
Akizungumza
mara baada ya kuwashwa umeme huo Mkuu wa shule hiyo Alidi Namulungu,
alisema kuwa moja ya sababu iliyowafanya wafanye vibaya katika Mtihani wa
Mwaka uliopita ni Wanafunzi kukosa Nishati mbadala ya kusomea hasa nyakati za
usiku kwani walikuwa wanatumia vibatari ambavyo vilikuwa vinamwanga hafifu
Alisema
upatikanaji wa umeme huo utakuwa mkombozi kwa walimu na wanafunzi hasa wakati
wa kujiandaa na mitihani yao kwa wanafunzi hao kuweza kusoma nyakati za
jioni pamoja na kuwasaidia katika suala la ulinzi na usalama shuleni hapo
No comments:
Post a Comment