Mbunge
wa Mtama, Nape Nnauye amejiuzulu Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Maliasili na Utalii.
Kujiuzulu kwake, kunatokana kile kinachoitwa, “Kugoma
kuondoa taarifa ya uchukuaji wa mashamba ya wawekezaji, kinyume na sheria.”
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii
zinasema, Nape amejiuzulu baada ya kutofautiana na serikali kuhusu ripoti ya
Kamati yake.
“Nape
alitaka ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii, iliombe Bunge kuundwa
kwa Kamati Teule ya Bunge ili kuchunguza utaratibu uliotumika wa kufuta
mashamba ya watu,” ameeleza mjumbe mmoja wa kamati hiyo.
Ameongeza,
“Serikali haitaki kuundwa kwa Kamati hiyo. Hivyo imeamua kuitumia Kamati ya
wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumlazimisha Nape kujiuzulu.”
Taarifa
kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii zinasema, tayari Nape
amemuandikia barua rasmi Spika kumjulisha kujiuzulu kwake.
Nape
alihuhutubia waandishi wa habari hapo jana akiwa chini ya vyombo vya usalama na kutetea
msimamo wake.
Kupatikana
kwa taarifa hizi kumekuja siku moja kabla ya Kamati yake kuwasilisha ripoti
yake na zinaeleza kuwa Kamati hiyo ilikuwa inaleta mapendekezo ya kuundwa kwa
Kamati Teule, jambo ambalo lilihofiwa kuwaumbua baadhi ya wakubwa.
Machi
mwaka 2017, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya uwaziri wa habari, utamaduni,
Sanaa na michezo.
Mbunge
huyo wa Mtama mkoani Lindi, alivuliwa wadhifa wake siku moja baada ya kupokea
ripoti ya Kamati ya uchunguzi juu ya tukio la uvamizi wa kituo cha televisheni
cha Clouds kwa kutumia silaha uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda.
Ripoti
ya kamati aliyoiunda Nape kuchunguza tukio hilo, ilithibitisha kuwa Makonda
alivamia kituo hicho majira ya saa 5 usiku wa Ijumaa ya tarehe 17 Machi 2017 na
alifanya uvamizi huo akitumia askari wenye silaha.
Nape
aliahidi kuifikisha ripoti yake kwa mamlaka ya juu yake ambapo haijajulikana mpaka sasa, ripoti hiyo
amekabidhiwa nani.
Nape
ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Idara ya Uenezi ya CCM, amesema atapata nafasi
nzuri ya kutumikia wananchi wa jimboni kwake baada ya kuachia nafasi hii.
No comments:
Post a Comment