Wednesday, February 27, 2019

MAJALIWA AKABIDHI JENERETA KITUO CHA AFYA MKOWE WILAYANI LUANGWA.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

Waziri Mkuu kasimu Majaliwa Akabidhi Jeneleta katika Kituo cha afya Mkowe kilichopo  katika kata ya Mkowe Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi litakalosaidi kufua Umeme wa Dharua kituoni hapo

Akizungumza na wananchi pamoja na wauguzi kituoni hapo  kwa Niaba ya Waziri Mkuu  Kasimu Majaliwa , wakati wa ghafla ya makabidhiano hayo Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Alisema amefurahishwa na maboresho yaliyofanyika katika kituo hiko kwa kuweza kufanya Upasuaji kwa akinamama Wajawazito. 

Alisema hali  hiyo inaonyesha  ni kwa namna gani dhamira ya uwekezaji huo umeweza kuleta tija katika kituo hicho.

Hata hivyo pamoja na mambo mengine Mgalu alilitaka shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Lindi kuendelea na uboreshaji wa upatikanaji wa umeme katika mkoa huo.

Awali akitoa taarifa ya kituo Mganga Mfawidhi wa  Kituo hicho Paulo Mbinga alisema kuwa kituo cha  Afya Mkowe ni miongoni mwa vituo vya Afya vilivyonufaika na mpango wa Serikali wa kuimarisha Miundombinu ya vituo vya Afya Nchini unaolenga kuviwezesha vituo vya Afya  kutoa huduma za Dharula kwa akina Mama Wajawazito   

Alisema Kituo hicho kwa sasa kinahudumia jumala ya Wananchi 5,224 wa Kata ya Mkowe pamoja na zile za jirani kama Chienjele, Nandagala, Likunja,Namalolo na  Mnacho ambapo jumla ya wagonjwa 74 hufika Kituoni hapo kwa siku kwa ajili ya kupatiwa Matibabu.

Mbinga aliongeza kuwa  kituo hicho kilipoanzishwa kilikuwa kinatoa huduma za nje OPD,  kulaza wagonjwa, kliniki kwa akina Mama wajawazito na Watoto, huduma za Uzazi wa Mpango pamoja na kujifungua akina Mama

Alisema kutokana na maboresho yaliyofanyika  hivi karibuni  kituo hicho kwa sasa kimeongeza  Huduma  za Damu salama, pamoja na Upasuaji kwa akina Mama  wajawazito.

Aidha, DKT Mbinga  alimshukuru Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa ambae pia ni Mbunge wa Jimbo hilo la Ruangwa kwa kuwasaidia jenereta katika Kituo hicho ambalo kwa kiasi kikubwa  litasaidia utoaji wa Huduma  kwa Wagonjwa Pindi umeme utakapokatika.

Hata hivyo DKT Mbinga alisema kuwa pamoja na kusaidia utowaji wa huduma pia jenereta hiyo litasaidia kuimarisha usalama wa Huduma za upasuaji katika Kituo


No comments:

Post a Comment