Thursday, February 28, 2019

NAPE APONGEZA KUWASHWA UMEME KIJIJI CHA TULIENI, LINDI.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

Kuzinduliwa kwa Umeme , kupitia mradi wa Umeme Vijijini (REA) katika Kijiji cha Tulieni kata ya Mtua Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani humo kunaweza kuwa Mwarobaini wa kumaliza changamoto ya upatikanaji wa Maji  inayowakabili wananchi kijijini hapo

Hayo yameelezwa na Mbunge Jimbo la Mtama Nape Nnauye wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa uwashaji wa umeme katika kata hiyo uliofanyika jana katika ofisi za  kijiji cha  Tulieni  na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji hicho Nape alisema kuwa kutokana na Kijiji  kuwa mlimani wakazi wa maeneo hayo hulazimika kushuka chini (mabondeni) kufuata huduma ya Maji katika mifereji na mito ambayo hata hivyo sio salama kwa afya zao

" Wakati wa Kampeni za uchaguzi mwaka 2015 kijiji hiki kilikuwa na Matatizo Makubwa mawili , moja bara bara ambalo limeshaanza kufanyiwa kazi na wakala wa bara bara mijini na vijijini (TARURA ) kwa kujenga barabra hiyo kwa kiwango cha lami lakini la pili uliposikia akina mama hawa wanapiga Vigere gere hapa tunatatizo kubwa la maji "Alisema Nape

"kutokana na Kijiji hiko kuwa  Mlimani  dawa pekee ya kuyaleta maji huku juu ilikuwa ni Umeme ndio maana tukasema tuanze na Umeme  alafu tuyavute maji kutoka  chini kuyaleta huku juu na awa akina mama waone wako Tanzania mzuri kwa kufungua maji kwenye mabomba" aliongeza Nape

Nape alifafanua kuwa uwekwaji wa umeme katika kijijini hapo kwa kiasi kikubwa utaleta chachu ya kuanzisha mchakato wa kutatua kero ya Upatikanaji wa maji

Akizungumza na Wananchi hao  Naibu Waziri Subira Mgalu  aliwaondoa wasiwasi wanakijiji hao juu ya Upatikanaji wa Maji kwani Serikali ilishaagiza kuzipa kipaumbele Taasisi muhimu kuunganisha umeme  katika maeneo yaliyopitiwa na Miradi ya Umeme Vijijini (REA) kama vile shule, Zahanati , miradi ya maji na Taasisi zingine kama hizo

Hata hivyo Mgalu alimuagiza Meneja wa Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Lindi Mhandisi Felisian Makota Kufikisha Umeme huo mara moja katika chanzo cha Maji Kijijini hapo pindibMchakato huo utakapoanza

Akisoma Taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa usambazaji Umeme Vijijini REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Lindi Mhandisi Felisian Makota alisema kuwa katika kutekeleza mradihuo kijiji cha Tulieni kimepangiwa kuwa na Wigo wa Msongo wa Umeme K .W  33 ambapo kazi hiyo imekamilika, ujenzi wa Line ndogo kilo mita 2 ambayo mpaka sasa tayari  mkandarasi amejenga kilomita 0.6  pamoja na mashine umba moja ambapo wateja wa awali wanataraji kuwa 14
 Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu (kati kati) na Mbunge Jimbo la Mtama Nape Nnauye (kushoto)
 
Wananchi wa Kijiji cha Tulieni kata ya Mtua Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi wakimsikiliza Naibu waziri wa Nishati wakati wa uzinduzi wa kuwasha umeme katika kijiji hicho.


No comments:

Post a Comment