Na
Hadija Hassan, Lindi.
Waziri
Mkuu Kasimu Majaliwa amemuagiza Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Ujenzi wa
Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, M/S National
Service Construction Department (SUMA JKT ) kutotumia vibarua wanaotoka nje ya
Wilaya hiyo na Badala yake wawatumie Vijana waliopo katika Halmashauri hiyo.
Majaliwa
aliitaka agizo hilo kwa Meja Atupele Mwamfupe Jana baada ya kutembelea na
kukagua eneo linalojengwa Ofisi hiyo ambapo alisema kuwa katika eneo hilo wapo
Vijana wa kutosha wa watakaoweza Kufanya Kazi kwa uweledi katika ujenzi huo.
Hata
hivyo Majaliwa alisema ili kuifanya Kazi hiyo iende kwa kasi na kukamilika
katika muda uliopangwa Ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za kuwatoa vibarua
nje ya Maeneo hayo ni vyema kutumia vibalua waliopo ndani ya Wilaya hiyo.
Awali
akisoma taarifa ya Mradi huo Mbele ya Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa, Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri hiyo ya Ruangwa, Andrew Chezue alisema kuwa Mradi huo
utagharimu Tsh. Bilioni 3,777,831,596.00 na unasimamiwa na Mtaalamu Mshauri M/S
Bureau for Industrial Cooperation (BICO) kwa Mkataba wa Tsh. Milioni
16,205,000.00
Chezue
alisema mradi huo umeanza rasmi mwezi Juni Mwaka huu wa 2019, na unatarajiwa
kukamilika mwezi juni Mwaka 2020 ambapo lengo lake kubwa ni kuboresha mazingira
ya kufanyia Kazi ikiwa pamoja na kuwa na jengo bora na imara ambalo litatumika
katika Shughuli Mbali mbali za Kiserikali.
Hata
hivyo Chezue alibainisha kuwa Mpaka sasa jumla ya Tsh. Milioni 500,000,000.00
zimeshatolewa na Serikali kuu kwa Mwaka wa fedha wa 2018/2019 ambazo zimetumika
kwa kumlipa Mkandarasi kwa ajili ya malipo ya awali (Advance payment), ili
aweze Kufanya stadi ya udongo pamoja na kusafisha eneo la mradi.
Nae
Meneja wa Kanda ya ujenzi wa Suma Jkt Kanda ya kusini, anaetekeleza mradi huo
wa ujenzi wa Ofisi Mpya ya Halmashauri, Meja Atupele Mwamfupe alisema kuwa
jengo hilo Litakuwa la ghorofa Moja ambalo
litahusisha vyumba 33 Chini na vyumba 29 Juu pamoja na kumbi mbili za
mikutano.
Alisema
mpaka sasa Kazi zilizokamilika ni pamoja na usafishaji wa eneo kwa ajili ya
ujenzi, upimaji wa sampuli ya udongo, uchimbaji wa kisima cha maji, ukusanyaji
wa Vifaa vya ujenzi eneo la Mradi, ujenzi wa uzio kuzunguka eneo la Mradi
pamoja na ufyatuaji wa matofali ambao unaendelea ambapo hadi sasa tofali 10,000
zimeshafyatuliwa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Rashidi Nakumbya aliishukuru
Serikali ya awamu ya tano kwa kuipatia Halmashauri hiyo fedha za ujenzi wa
Ofisi Mpya na ya kisasa Itakayokuwa na mchango Mkubwa katika kuongeza ufanisi
wa Kazi kwa watumishi wa Halmashauri hiyo.
NaKumbya
aliongeza kuwa Kutokuwa na Ofisi kubwa katika Halmashauri hiyo hivi sasa
kunasababisha mtawanyiko wa baadhi ya Idara kunakotokana na ukosefu wa majengo
hali ambayo wananchi hupata shida wanapokwenda kupata huduma.
Hata
hivyo alieleza changamoto nyingine kuwa ni kuwepo kwa Msongamano wa watumishi
kutumia Chumba kimoja baina ya Wakuu wa Idara na vitengo katika Idara jambo
ambalo linapelekea kupunguza ufanisi wa kazi.
Utayarishaji
wa eneo la ujenzi ukiwa unaendelea.
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi litakapokamilika.
PICHA ZOTE NA HADIJA HASSAN.