Thursday, February 28, 2019
Waziri Kamwelwe asifu utendaji kazi wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi. Isack Kamwele amepongeza utendaji kazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Mhe. Kamwele alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea Ofisi za TMA, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, tarehe 27 Februari 2019 na alipata taarifa ya utendaji kazi wa mamlaka na kutembelea baadhi ya sehemu za kazi kabla ya kuzungumza na wafanyakazi. Mhe. Kamwele alipokelewa na uongozi na menejiment ya TMA, ikiongonzwa na mwenyekiti wa bodi ya ushauri Dkt. Buruhani Nyenzi na kaimu mkurugenzi mkuu Dkt. Ladislaus Chang’a. Kat
“Nawapongeza TMA kwa umakini na utekelezaji wa majukumu yenu, nakiri kusema ni moja ya taasisi makini kati ya taasisi zilizo chini ya wizara yangu nilizo tembelea”. Alizungumza mhe. Kamwele
Aidha, mhe. Kamwele alisisitiza kuboresha mfumo wa ushirikishwaji wa wadau na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa, akitolea mfano mafuriko yaliyo bomoa barabara eneo la Dumila, kuwa baada ya kufuatilia taarifa za hali ya hewa waligundua TMA ilitoa taarifa hizo siku mbili kabla ya tukio na kuonesha rangi nyekundu yenye kumaanisha tahadhari kwa maeneo ya Kilindi lakini taarifa hiyo haikuwafikia walengwa.
Mhe. Kamwele alimalizia kwa kuahidi kutatua changamoto zinazoikabili TMA zikiwemo uhitaji wa ongezeko la vituo vya hali ya hewa, mitambo ya hali ya hewa, kupatikana kwa jengo la kituo kikuu cha utabiri n.k
Akitoa salamu za shukrani kwa upande wa TMA, mkurugenzi wa ofisi ya TMA Zanzibar, Bw. Mohamed Ngwali alimshukuru mhe. Waziri kwa pongezi sambamba na kutembelea na kuona shughuli zinazofanywa na TMA, na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa .
Imetolewa:
Ofisi ya Uhusiano
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
DC BAGAMOYO ATAKA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA WOTE KURIPOTI SHULE IFIKAPO JUMATATU MACH 04.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa, akishiriki ujenzi wa vymba vya madarasa shule ya sekondari Pera Halmashauri ya Chalinze, aliyesimama kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Saidi Zikatimu.
............................
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawaamewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka shule watoto wote
waliofaulu kuingia kidato cha kwanza ifikapo jumatatu ya tarehe 04 Mach 2019.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa tamko hilo wakati
akizungumza na viongozi wa kata na tarafa katika Halmashauri ya Chalinze na
kuwataka viongozi hao wasimamie maagizo hayo.
Tamko hilo limekuja baada ya shughuli za ujenzi
wa vyumba vya madarasa zikiendelea wilaya yote ya Bagamoyo lengo likiwa ni
kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakaekosa masomo kwasababu ya upungufu wa vyumba
vya madarasa.
Katika ziara yake hiyo ya kukagua ujenzi wa
vyumba vya madarasa, Mkuu huyo wa wilaya ameshiriki shughuli za ujenzi katika
shule ya Sekondari Pera kata ya Pera Halmashauri ya Chalinze ambapo ujenzi wake
unaendelea.
Wakati hyuo huo Mkuu huyo wa wilaya Zainabu
Kawawa amesema kila mzazi anapaswa kusaini mkataba maalum wa kuthibitisha kuwa
mtoto wake atasoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne bila ya kukosa.
Katika zoezi hilo la kusaini mikataba amewaagiza
maafisa tarafa kusimamia na mzazi au mlezi atakaekwenda kinyume atachukuliwa
hatua za kisheria.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa kata na tarafa na wanachi wanaoshiriki ujenzi wa shule ya sekondari Pera Halmashauri ya Chalinze, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Saidi Zikatimu.
NAPE APONGEZA KUWASHWA UMEME KIJIJI CHA TULIENI, LINDI.
NA
HADIJA HASSAN, LINDI.
Kuzinduliwa
kwa Umeme , kupitia mradi wa Umeme Vijijini (REA) katika Kijiji cha Tulieni
kata ya Mtua Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani humo kunaweza kuwa
Mwarobaini wa kumaliza changamoto ya upatikanaji wa Maji inayowakabili
wananchi kijijini hapo
Hayo
yameelezwa na Mbunge Jimbo la Mtama Nape Nnauye wakati wa hafla fupi ya
uzinduzi wa uwashaji wa umeme katika kata hiyo uliofanyika jana katika ofisi za
kijiji cha Tulieni na Naibu Waziri
wa Nishati Subira Mgalu
Akizungumza
kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji hicho Nape alisema kuwa kutokana na
Kijiji kuwa mlimani wakazi wa maeneo hayo hulazimika kushuka chini
(mabondeni) kufuata huduma ya Maji katika mifereji na mito ambayo hata hivyo
sio salama kwa afya zao
"
Wakati wa Kampeni za uchaguzi mwaka 2015 kijiji hiki kilikuwa na Matatizo
Makubwa mawili , moja bara bara ambalo limeshaanza kufanyiwa kazi na wakala wa
bara bara mijini na vijijini (TARURA ) kwa kujenga barabra hiyo kwa kiwango cha
lami lakini la pili uliposikia akina mama hawa wanapiga Vigere gere hapa
tunatatizo kubwa la maji "Alisema Nape
"kutokana
na Kijiji hiko kuwa Mlimani dawa pekee ya kuyaleta maji huku juu
ilikuwa ni Umeme ndio maana tukasema tuanze na Umeme alafu tuyavute maji
kutoka chini kuyaleta huku juu na awa akina mama waone wako Tanzania
mzuri kwa kufungua maji kwenye mabomba" aliongeza Nape
Nape
alifafanua kuwa uwekwaji wa umeme katika kijijini hapo kwa kiasi kikubwa
utaleta chachu ya kuanzisha mchakato wa kutatua kero ya Upatikanaji wa maji
Akizungumza
na Wananchi hao Naibu Waziri Subira Mgalu aliwaondoa wasiwasi
wanakijiji hao juu ya Upatikanaji wa Maji kwani Serikali ilishaagiza kuzipa
kipaumbele Taasisi muhimu kuunganisha umeme katika maeneo yaliyopitiwa na
Miradi ya Umeme Vijijini (REA) kama vile shule, Zahanati , miradi ya maji na
Taasisi zingine kama hizo
Hata
hivyo Mgalu alimuagiza Meneja wa Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Lindi
Mhandisi Felisian Makota Kufikisha Umeme huo mara moja katika chanzo cha Maji
Kijijini hapo pindibMchakato huo utakapoanza
Akisoma
Taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa usambazaji Umeme Vijijini REA awamu ya tatu
mzunguko wa kwanza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Lindi Mhandisi Felisian Makota
alisema kuwa katika kutekeleza mradihuo kijiji cha Tulieni kimepangiwa kuwa na
Wigo wa Msongo wa Umeme K .W 33 ambapo kazi hiyo imekamilika, ujenzi wa
Line ndogo kilo mita 2 ambayo mpaka sasa tayari mkandarasi amejenga
kilomita 0.6 pamoja na mashine umba moja ambapo wateja wa awali
wanataraji kuwa 14
Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu (kati kati) na Mbunge Jimbo la Mtama Nape Nnauye (kushoto)
Wananchi wa Kijiji cha Tulieni kata ya Mtua Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi wakimsikiliza Naibu waziri wa Nishati wakati wa uzinduzi wa kuwasha umeme katika kijiji hicho.
Wananchi wa Kijiji cha Tulieni kata ya Mtua Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi wakimsikiliza Naibu waziri wa Nishati wakati wa uzinduzi wa kuwasha umeme katika kijiji hicho.
Uzinduzi wa kampeni ya ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili wa kingono wafana dar…viongozi wa dini, jamii yaombwa kumlinda mtoto
Mgeni katika shughuli hiyo, Mkuu wa Dawati la kijinsia kutoka makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, DCP Maria Nzuki akielezea jambo katika Kampeni hiyo. |
Mkurugenzi mtendaji Lilian Liundii akifafanua jambo |
Mkurugenzi akiiwa na mgeni rasmi katika kampenii hiyo. |
Na Selemani Magali
Kampeni
ya ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili wa kingono- “1-5-5 namlinda” yenye kauli
mbiu “mlinde mtoto afurahie utoto wake,
ujana wake na uzee wake” imezinduliwa jana huku viongozi
wa kidini na jamii kwa ujumla wakitakiwa kutumia majukwaa yao kuhubri juu ya
umuhimu wa kuwalinda watoto dhidi ya vitendo viovu vya ukatili wa kingono,
ikisisitizwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia kuwalinda watoto.
Akizungumza
katika ufunguzi wa Kampeni hiyo iliyolenga kuamsha Jamii kushiriki katika
kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vyote vya Kingono, Mkuu wa Dawati la
kijinsia kutoka makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, DCP Maria
Nzuki amesema viongozi wa dinii wanayo nafasi ya kupunguza ukatili huo.
“Viongozi wa kiroho wanayo nafasi ya
kutokomeza ukatili wa kingono, wao wanawatu wengi na wanaaminika, wakisema
jambo waumini wao watalipokea na kulifanyia kazi…basi chukueni na hili
mkalifanyie kazi, mara nyingi watu hupendwa kukumbushwa kumbushwa…kumbusheni basi
na hili huwenda kukawa na manufaa.” Aliongeza DCP Nzuki.
Aidha
DCP Nzuki amewaomba jamii kuwalinda watoto kwa kutoa taarifa mapema mara tu
waonapo ona viashiria vya ukatili wa Kingono, ikiwamo watoto wa shule kuingia
quest, kulala katika chumba au nyumba ya msela kisha wakakaa muda mrefu, na
matendo yanayofanana na hayo.
Akielezea hali ya ukatilii wa Kingono
Tanzania DCP Nzuki amesema kumekuwa na ongezeko ambapo sasa kila sehemu ya
yenye wanawake watatu mmoja tayali amewahi kufanyiwa vitendo hivyo, na kuongeza
kuwa tatizo ni kubwa linalohitaji nguvu ya pamoja kuliondoa.
Akizungumzia
hatua mbalimbali zinazochukuliiiiwa na Serikali kupambana na hali hiyo, DCP
Nzuki amesema kwa upande wa Serikali
kupitia Jeshi la polisi tayari jitihada mbali mbali zinachukuliwa
ikiwamo kuweka madawati ya kijinsia katika vituo vya polisi, kuweka vituo vya
mkono kwa mkono katika baadhi ya hosptali (one stop centers) pamoja na kuongeza
usiri kwa watoa taarifa.
Aidha DCP nzuki amewaka wazazi na
walezi wa watoto kufahamu kuwa jukumu la kumlea mototo ni la kwao na wanapaswa
kuhakikisha wanamlinda mototo na vitendo vyote vya ukatili wa kingono.
Amesema wazazi wanajukumu la kuwa
karibu na watoto wao na kuzungumza madhara ya ukatili wa kingono ambapo
itawasaidia watoto kutoa taarifa wakati wanapofanyiwa vitendo hivyo na
watu wasio julikana.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi akielezea kampenii
hiyo, amesema Kampeni hii imelenga kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya athari
za ukatili wa kingono kwa watoto na umuhimu wa kuwalinda dhidi aina hiyo ya
ukatili, kutathmini na kuibua mijadala katika jamii juu ya hali halisi ya
ukatili wa kingono, kuhamasisha jamii kuzuia vitendo hivi visitokee na kutoa
taarifa mara waonapo matukio hayo ya
ukatili wa kingono kwa watoto ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua stahiki.
Amesema Vitendo
hivi vinarudisha nyuma maendeleo ya mtoto na taifa kwa ujumla. Miongoni mwa
athari zitokanazo na ukatili wa kingono dhidi ya watoto ni pamoja na watoto
kuathirika kisaikolojia, maambukizi ya magonjwa ya zinaa na UKIMWI, mimba za utotoni,
na kubwa zaidi ni kuhatarisha ustawi wa taifa na kuchochea uongezeko la vitendo
hivi katika jamii.
Ukatili
wa Kingono Tanzania bado ni tatiizo sugu, kwa mujibu wa tafitii inaoonyesha
kuwa mnamo mwaka 2011, katika wasichana watatu mmoja amefanyiwa na mmoja kati
ya wavulana saba wamekutana na ukatili wa kingono kabla ya kutimiza miaka 18.
Hata hivyo, kulingana na utafiti huo, wengi wa
watoto hawatoi taarifa juu ya vitendo hivyo,
wachache wanatafuta huduma na wachache
zaidi wanafanikiwa kupata matibabu au msaada wanapotoa taarifa ya matukio hayo.
Pia, ripoti iliyotolewa na Kituo cha sheria na
haki za binadamu (LHRC) zinaonyesha kuwa matukio ya ukatili wa kingono miongoni
mwa watoto yanaongezeka nchini.
Kulingana na ripoti hiyo iliyotolewa Juni
2018, wastani wa watoto 394 wamebakwa kila mwezi katika maeneo mbalimbali Tanzania
bara, huku ulawiti wa watoto ukiongezeka kutoka matukio 12 kwa kipindi cha Januari hadi Juni
2017 hadi matukio 533 kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2018, na mikoa inayoongoza
kwa matukio hayo ni Dar es salaam na Iringa.
Ends
Subscribe to:
Posts (Atom)