Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kulia kwake) wakizungumza na
wakagonjwa wakati walipotembelea hospitali ya wilaya ya Mpanda wakiwa katika
siku ya kwanza ya ziara ya mkoa wa Katavi leo Agosti 21, 2016. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
.......................................................................................
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri nchini kuwachukulia
hatua watumishi wote wa sekta ya afya wanaojihusisha na wizi wa dawa.
“Fuatilieni na kuwachukulia hatua
watumishi wa Zahanati wanaoiba dawa. Hawa hawana nafasi ya kuendelea kufanya
kazi kwa sababu ni wauaji,” alisema.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo
jana jioni (Jumamosi, Agosti 20, 2016) wakati akipokea taarifa ya mkoa wa
Katavi mara baada ya kuwasili mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Alisema kila kiongozi kwenye eneo
lake ahakikishe dawa zinazopelekwa na Serikali kwa ajili ya kuwahudumia
wananchi zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Pia ameitaka Bohari Kuu ya Dawa
(MSD) kujenga duka la dawa mkoani Katavi kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji
wa dawa katika mkoa huu pamoja na mikoa jirani.
Wakati huo huo Waziri Mkuu
aliwataka Waratibu wa Elimu katika ngazi ya Kata na Wakuu wa shule za sekondari
wasiokuwa na shahada waende wakasome kama wanahitaji kuendelea kuwa na wadhifa
huo.
Alisema Mratibu wa Elimu katika
ngazi ya Kata ni lazima awe na shahada ili aweze kutekeleza majukumu yake ya
kusimamia utolewaji wa elimu katika shule za sekondari na msingi.
Kwa upande wa walimu wakuu katika
shule za msingi, Waziri Mkuu alisema ni lazima wawe na diploma, hivyo aliwataka
walimu wakuu wote wasiokuwa na diploma kwenda kusoma kabla hawajaondolewa
kwenye wadhifa huo.
Alisema Serikali imetenga zaidi
ya sh. bilioni tano kwa mwezi ambazo ni posho ya madaraka, ambapo Waratibu
Elimu Kata wanapewa sh 250,000 kwa mwezi huku Wakuu wa shule za sekondari na
walimu wakuu katika shule za msingi wanapewa sh. 200,000.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja
Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga alisema mkoa umeendelea kuongeza bajeti
ya dawa ili kuhakikisha dawa zinapatikana katika ngazi zote za kutolea huduma.
“Mwaka 2012 bajeti ya dawa na
vifaa tiba ilikuwa sh. Milioni 558 ambayo ilitosheleza upatikanaji wa dawa na
vifaa tiba kwa asilimia 70. Katika bajeti ya mwaka 2016/2017 mkoa umetengewa
jumla ya sh bilioni 1.3 ambayo tunaamini itamaliza tatizo la upatikanaji wa
dawa na vifaa tiba,” alisema.
Mkuu huyo wa mkoa alisema mfumo
mpya wa usambazaji dawa kupitia MSD umesaidia dawa, vifaa tiba na vitendanishi
kupelekwa moja kwa moja hadi katika ngazi ya zahanati hali iliyosaidia
dawa kufika kwenye vituoZIARA YA vya kutolea huduma kwa asilimia 100.
Mapema leo Waziri Mkuu amefanya
ziara katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambapo amesema Serikali
itahakikisha hospitali hiyo inaongezewa huduma zaidi kwa sababu ni ya wilaya
ila inahudumia wagonjwa wa mkoa wote.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea hospitali ya wilaya ya Mpanda akiwa katika
siku ya kwanza ya ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kulia kwake) wakizungumza na
wakagonjwa wakati walipotembelea hospitali ya wilaya ya Mpanda wakiwa katika
siku ya kwanza ya ziara ya mkoa w Katazi Agosti 21, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majlaiwa na mkewe Mary wakitazama watoto mapacha wa kiume
waliozaliwa na Bi Sikudhani Raashidi usiku wa kuamkia Agosti 21, 2016
katika hospitali ya wilaya ya Mpanda wakati walipoiembelea Agosti21, 2016.
Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mbunge wa Viti Maalum, Anna Lupembe. (Picha na ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa na Mkewe Mary wakimtazama mtoto Nchambi Peter aliyeungua
moto wakati walipotemblea hospitali ya wilaya ya Mpanda Agosti 21, 2016.
Kulia ni Mam wa mtoto huyo, Dotto Makengele. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
No comments:
Post a Comment