Kamanda wa Polisi kanda
maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa
Polisi SP. Simon Sirro akiwaonyesha
waandishi wa habari fulana yenye maandishi
ya UKUTA. zilizo andaliwa kwaajili ya maandamano.
Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi SP. Simon Sirro
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matukio mbalimbali ikiwemo namna
walivyojipanga kuzuia maandamano ya UKUTA yaliyopangwa kufanyika septemba 1, mwaka huu.
.....................................................................................
JESHI la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya Chama cha
Demokrasia Maendeleo n (CHADEMA) yanayopangwa kufanyika Septemba 1 mwaka
huu.
Maandamano
hayo yaliyopewa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania, (UKUTA)
ambapo wanachama wake wanataka kuingia mitaani kupinga kile wanachokiita
ukandamizaji wa demokrasia nchini Tanzania.
Kauli hiyo
imetolewa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi,
CP Simon Sirro na kuongeza kuwa maandamano hayo hayatafanyika na kwamba jeshi
la polisi limejipanga kuzuia aina yoyote itakayo ashiria kuwepo kwa maandamano hayo.
Kamanda
Sirro amesema kuwa hakuna habari ya Ukuta na hakuna mtu atakayedhubutu kuingia
barabarani kutokana na jeshi la polisi lilivyojipanga kuhakikisha wananchi
wanafanya shughuli zao bila kuingiliwa na kitu chochote.
Alisema
kuwa utaratibu wa kufanya mikutano ya siasa umeelezwa hivyo kufanya mikutano
bila kufuata utaratibu jambo hilo halitaruhusiwa.
Kamishina
Sirro amesema kuwa kikundi/watu wanaotaka kutumia siasa katika kuvunja
Amani kwa Dar es Salaam hakuna nafasi hiyo kutokana na jeshi la polisi
lilivyojipanga.
Aidha,
Kamanda Sirro alisema Jeshi kufuatia maandalizi yanayofanywa na wale wanaotaka
kuvunja sheria katikakufanya maandamano hayo.
Jeshi la
Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam,
Agosti 20 majira ya saa 12:00 jioni lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa
maeneo ya mtaa wa Ufipa Kinondoni kuna duka linauza flana rangi mbalimbali
zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’
rangi nyeupe idadi yake 28, rangi nyekundu fulana 18 zenye maneno ‘UKUTA’
fulana 6 za Kakhi zenye maneno ‘’UKUTA’ Na fulana zingine rangi
nyeusi 23 zenye maneno ’’UKUTA’’.
Aidha Polisi baada ya
kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa Yoram Sethy
Mbyelllah (42) mfanyabiashara, mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo
dukani kwake. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na baada ya upelelezi kukamilika
atafikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment