Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye
akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, wakati akitangaza kuzifungia
radio mbili kwa muda usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi na kuvirusha
hewani ambavyo vinaashiria uchochezi.
...................................................................................................................
WAZIRI wa Habari,
Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye amezifungia radio mbili kwa muda
usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi ambavyo vimerushwa hewani
vinavyoashiria uchochezi.
Akizungumza na waandishi
wa habari, Waziri Nape amesema kuwa uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikiwa
baaa ya kujirdhisha kuwa kipindi cha Matukio kilichorushwa Agosti 25, 2016 muda
wa saa 2 usiku hadi saa 3 na kituo cha utangazji cha Radio 5 pamoja na kipindi
cha Morning Magic katika kipengele cha Kupaka Rangi Agosti 17 vilikuwa na
maudhui ya uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa Amani.
Nape amesema kuwa
kufuatia hilo amevifungia kwa muda usiojulikana kwani wamekiuka masharti ya
kanuni ya 5 (a, b, c na d) , kanuni ya 6 (2a, b na c) na kanuni ya 218 ya
huduma za utangazaji ya mwaka 2005.
Wakati vituo hivyo
vikifungiwa kwa muda usiojulikana kamati ya maudhui imepewa jukuu la kuviita na
kusikiliza kwa kina Zaidi utetezi wao na ni hatua gani zaidi ya kuchukua dhidi
yao kwa mujibu wa kanuni ya huduma za utangazaji.
Nape ameendelea
kuvitahadhalisha vyombo mbalimbali vya habari kutoshawishika kuvunja sheria na
kanuni zinazoongoza tasnia ya habari ili kulinda heshima ya tasnia yetu na
wakati huo kuhakikisha nchi inabaki na Amani, Mshikamano na Umoja.
CHANZO, jiachie blog.
No comments:
Post a Comment